WAANDISHI WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA WELEDI NA KUFUATA SHERIA YA HABARI ,SAMBAMBA NA KUONGEZA VIWANGO VYAO VYA ELIMU

Wakili msomi James Marenga na Mwanahabari mwandamizi akizungumza na waandishi wa habari katika semina iliyoandaliwa na Taasisi ya habari kusini mwa Afrika( MISA-TAN)kwa kushirikiana na Shirika la Kijerumani linaloshughulika na Utawala bora la Friedrich Ebert Stiftung.Picha na Vero Ignatus Blog.


Waandishi wa habari Godwin Charles kutoka Idea FM Radio iliyopo mkoani Arusha ,akifuatiwa na mwandishi wa habari kutoka Radio five Tonnie Kaisoi,Jamila Omari kutoka kituo cha lunicha cha channel ten,pamoja na Winnie Juma kituo cha radio cha MJ FM, cha jijini Arusha wakifuatilia mada zinazoendelea katika semina hiyo.Picha na Vero Ignatus Blog.
 Waandishi wa habari Charles Masanyika kutoka kituo cha Luninga cha ITV pamoja na Mary Mwita kutoka gazeti la Tanzania Daima wakifuatilia mada mbalilmbali katika semina hiyo iliyofanyika katika hotel ya Impala iliyopo katika jiji la Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.

 Wakili msomi James Marenga na Mwanahabari mwandamizi  akizungumza na waandishi wa habari juu ya sheria ya huduma ya habari na sheria nyingine ya haki ya kupata taarifa ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.Picha na Vero Ignarus Blog.

Mwandishi wa habari na mmiliki wa( Vero Ignatus Blog) Vero Ignatus akiwa pamoja na Tumaini Mafie kutoka Safina Radio FM iliyopo katika jiji la Arusha wakifuatilia kwa makini kile kinachoendelkea katika semina hiyo.



Waandishi wahabari wakifuatilia kwa makini semina inayoendelea
Khalifa Mshana mwandishi wa habari( TBC)akitoa shukrani kwa niaba ya waandishi wa habari
 Mwandishi wa habari za mtandaoni (Blogger)Oscar akipokea cheti baada ya kuhitimu mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)
 Mwandishi wa habari kutoka gazeti la majira mkoani Manyara Mary Margwe akipokea cheti mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)

 Mwandishi wa habari kutoka gazeti la jambo leo mkoa wa Manyara Julieth Peter akipokea cheti mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)
  Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Luninga cha Chanel ten ,Jamila Omary akipokea cheti baada ya kuhitimu mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)

 Mwandishi wa habari za mtandaoni na mmiliki wa Vero Ignatus Blog
akipokea cheti baada ya kuhitimu mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)

 Mwandishi wa habari za mtandaoni (Blogger)Msumba news akipokea cheti baada ya kuhitimu mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)



Na.Vero Ignatus ,Arusha

Waandishi wa habari wametakiwa kufuata sheria ya huduma ya habari ikiwa ni pamoja na kuboresha elimu zao ili kutimiza matakwa ya sheria hiyo

Hayo yamesemwa na Wakili msomi James Marenga na Mwanahabari mwandamizi katika semina ya siku mbili  iliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya  habari kusini mwa Afrika( MISA-TAN)kwa kushirikiana na Shirika la Kijerumani linaloshughulika na Utawala bora la Friedrich Ebert Stiftung kuhusiana na sheria ya huduma ya habari

Marenga amesema kuwa lengo la mafunzo haya yaliyoshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa minne ya kanda ya kaskazini ni kuhusiana na sheria ambazo ni za habari ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake za mwaka 2017ambapo sheria hii inagusa sana kazi za waandishi wa habari ambapo inatambua nani ni mwandishi na kwa vigezo gani.

Amesema kuwa kanuni zinaelekeza kuwa ilimtu aweze kuwa ni mwandishi wa habari au chombo cha habari kinachotaka kuajiri anatakiwa kuajiri watu wenye viwaango na vigezo vinavyohitajika awe na elimu ya kuanzia ya kiwango cha stashahada(diploma) 

Hata hivyo amesema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuandika habari zao kwa kufuata taaluma nawaepuke kuandika habari za uchochezi ili kufuata kanuni na taratibu za sheria mpya ambapo inatoa kanuni na taratibu za uandishi ambapo hapio awali hazikuwepo lakini sheria hii imeweka makosa ambayao ni changamoto kwa wanahabari.

Hata hivyo akitoa shukrani kwaniaba ya waandishi mshiriki wa semina hiyo Khalifa Mshana amewataka wanahabari kuwaelimisha wengine juu ya sheria hiyo ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazoweza kutokea kwa ukiukwaji wa sheria hiyo

Sambamba na hilo semina hiyo imewashirikisha waandishi kutoka mikoa minne ya kanda ya kaskazini ikiwemo Arusha,Tanga,Manyara pamoja na Kilimanjaro.

No comments