Nyanza Fc watinga fainali ligi ya mkoa wa Manyara kwa kishindo

Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Timu ya nyanza fc imefanikiwa kuingia fainali ligi ya mkoa wa manyara  baada ya kuifunga timu ya magugu Rangers magoli 4 kwa moja 

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu wa shekh Abeid Karume jijini Arusha  badala ya kuchezwa katika mji wa mererani na hili ni kutokana  na uongozi wa ligi hiyo kuiamisha mechi hiyo kwenye uwanjani huo kuhofia fujo ya mashabiki.

Kwa upande wake msemaji wa timu wa nyanza fc bwana Peter Mwaluko amesema kuwa amefurahishwa sana na hatua ilifikia ya timu yake ya  nyanza .

Aidha mwaluko amewataja mashabiki wa nyanza fc kujitokeza kwa wingi kuishamgilia timu hiyo Siku ya fainali kwani wanamatumaini makubwa ya kuibuka na ubingwa ambapo mchezo huo wa fainali utakuwa kati ya Siku ya jumatano au alhamisi wiki hii.

No comments