Nyanza Fc wakabidhiwa zawadi kwa ushindi walioupata wa kuwa mabingwa wa mkoa wa Manyara

Mdhanini mkuu wa Nyanza Fc Elias Maduhu akimkabidhi mmoja wa wachezaji kitita cha pesa kama motisha kwa kazi nzuri walioifanya.


Na.Vero Ignatus ,Manyara.

Siku chache  baada ya kutwaa kombe la la daraja la tatu mkoa wa manyara

Mdhamini mkuu wa timu hivyo Elias Maduhu ameamua kuwafanyia surprise wachezaji kwa kuwapatia kitita cha pesa kama motisha kama pongezi kwao.

Akikabidhi zawadi hizo kwa wachezaji ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mazubu Grand Hotel iliyopo Mererani aliwataka vijana yao kutumia pesa hizo walizopewa vizuri ili iwe kumbumbu nzuri maishani mwao.

Awali kwenye sherehe za kukabidhi kombe kwa washindi hao Mkurugenzi huyo aliwataka viongozi wa vilabu vilivyoshiriki ligi hivyo kuvunja makundi na kuwa kitu  kimoja kuosapoti klabu ya nyanza Fc katika mashindano ya kanda kwani ndiyo wawakilishi wa mkoa wa Manyara.

Sambamba na hilo Mdhamini  huyo alitumia muda huo kuvunja kwambi ili kuwapa wachezaji mapumziko ya wiki tatu kabla ya kurudi kujiandaa na ligi daraja la tatu ngazi ya kanda.

Kwa upande wake mkuu wa kituo cha pilisi cha mji mdogo wa Mererani Acp Evarist Makala amewaomba wadau wa soka kuondoa tofauti walizokuwa wafuate sheria za nchi wailinde amani iliyopo kwani ikivunjika hakuna anayeweza kuirudisha

Licha ya kufungwa kwenye fainali hiyo Katibu Wa Songa Fc Agenyo Sigo amesema kuwa timu itaendelea kukaa kambini huku wakifanya marekebisho maxhache yaliyijitokeza kwenye kikosi chao ili kujiweka fiti Kwa msimu ujao Wa ligi daraja LA tatu ngazi ya mkoa.

No comments