JUMUIKO LA MALIASILI TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA RAIS TAMISEMI WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NA WADAU WENGINE.
Mratibu wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI), Bw. Sanford Kway akitoa mada kwa wanahabari pamoja na washiriki wa mafunzo ya mabadiliko ya Tabianchi pamoja nawadau mbalimbali wa mazingira waliohudhuria katika mafunzo hayo yaliofanyika katika Ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Sokoine mjini Dodoma leo.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo mjini Dodoma leo
Mratibu, Mawasiliano na ushawishi Jumuiko la Maliasili Tanzania, Sophia Masuka akitolea ufafanuzi kuhusu kazi za taasisi ya TNRf inavyoshirikiana na serikali kupitia TAMISEMI ili kuweza kupambana na mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.
Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Paul Dotto Kuhenga akitoa mada kwa waandishi wa habari pamoja na wadau wengine kuhusu mabadiliko ya Tabianchi na jinsi ya waandishi wa habari kuandika habari zinazohusiana na mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza kupunguza athari za mabadiliko hayo'
Mwandishi wa habari kutoka (TBC)Akiwa anauliza swali katika mafunzo yanayoendelea leo Dodoma
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika Picha ya pamoja
Na,Vero Ignatus .Dodoma
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (0R-TAMISEMI
)kwa kushirikiana Asasi ya kiraia ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) wameandaa mafunzo Kwa waandishi wa habari,Maafisa mawasiliano na Tehama kutoka kwenye idara za Serikali kuhusu mradi wa kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo mratibu wa Mradi wa Kuhimili mabadiliko ya tabianchi ambaye pia ni Afisa Misitu Mkuu (OR-TAMISEMI
) Bw.Sanford Kway amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitano unaolenga kuwekeza kwenye miradi ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika Halmashauri za Wilaya15 ambapo Kwa sasa unafanyika Kwa majaribio katika Halmashauri 3 ambazo ni Monduli,Longido na Ngorongoro .
Halmashauri hizo kwa upande wa Tanzania Bara ni Pamoja na Halmashauri za Wilaya za Bahi,Iramba,Kilwa,Kiteto,Kondoa,Manyoni,Mbulu,Mpwapwa,
Pangani,Same,Siha na Simanjiro.
Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza umeanza mwaka 2016 -2018 upo chini ya Uratibu wa OR - TAMISEMI na utalaamu wa kiufundi unatolewa na Taasisi imataifa ya Mazingira na maendeleo (IIED).
No comments