RC Gambo Ashiriki ibada ya Ijumaa kuu Arusha
Na.Vero Ignatus .Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Ameshiriki Ibada ya Ijumaa kuu ya PASAKA iliyoandaliwa na umoja wa makanisa ya Kikristo katika viwanja Vya Shehe amr Abeid Arusha kwa ajili ya ushindi wa Yesu kristo Bwana wao dhidi ya dhambi na uchungu na kumbukumbu ya siku ya mateso ya YESU.
Akizungumza na wakristo hao pamoja na Watanzania Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kilichopo ni kudumisha amani na upendo kila siku hku akieleza kusikitishwa na tukio la askari waliouwawa na majambazi mkoani Pwani na tukio la Kupigwa risasi kwa kijana wa umri wa miaka 15 katika kijiji cha lenjani kata Ya Lemanyata wilaya ya Arumeru
Mh Gambo amesema kuwa matukio hayo hayatavumikia na kuwaomba viongozi wa dini pamoja na wananchi kukemea vitendo hivyo vya kikatili ambavyo vinahuzunisha wananchi na kuwaasa vyombo vya dola kuacha kutumia nguvu zilizopitiliza na amewahakikishia wananchi kuwa suala hilo litashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Hata hivyo Mh Gambo amejitolea kushiriki chakula na watoto Yatima ambapo ametoa kiasi cha shilinngi laki 5 kwa ajili ya kufurahia na nao katika vituo vyao jambo ambalo amesema kuwa kila mtu anapaswa kutenda wema kwa kuwakumbuka wale wasionavyo wajisikie wanavyo .
Katika mahubiri ya Ibada hiyo ya pasaka Kwa wakristo ambayo yametolewa na Askofu mkuu wa Makanisa ya KKKT Mch Solomoni Masangwe amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuungana na wakristo kuombea nchi pamoja na siku ya kuteswa kwa bwana wao yesu kristo.
Askofu Solomoni amesema sikuu hii ya pasaka iwakumbushe wakristo pamoja na watanzania kufanya yaliyomema kwa kupeana taarifa njema amnazo zitaweza kujenga nchi na kulinda amani.



No comments