Nyanza Fc ya Mererani Mabingwa wapya wa mkoa wa Manyara

Mdhamini mkuu wa timu ya Nyanza Fc kutoka Mkoani Manyara Elias Maduhu akizungumza Mara baada ya Timu hiyo kushinda.Picha na Vero Ignatius Blog
Shangwe zikiendelea baada ya kushinda Timu ya Nyanza FC.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mashabiki wa Nyanza Fc wakifanya yao baada ya Timu hiyo kujinyakulia ushindi dhidi ya Songa Fc katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid.Picha na Vero Ignatus BlogNa.Vero Igantus ,Arusha
Timu ya Nyanza Fc ya mji wa Meretani imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa Wa Manyara baada ya kuofunga timu ya Songa Fc Kwa mkwaju ya penati 5 Kwa 4.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja Wa shekhe Amri Abeid kutokana na kuhamishwa kutoka mji wa Mererani Kwa sababu za kiusalama
Timu hiyo itauwakilisha mkoa wa Manyara katika mashindano ya ligi daraja la 3 ngazi ya kanda ya kaskazini.
Licha ya kufungwa kwenye fainali hiyo Katibu Wa Songa Fc Agenyo Sigo amesema kuwa timu itaendelea kukaa kambini huku wakifanya marekebisho machache yaliyojitokeza kwenye kikosi chao ili kujiweka fiti Kwa msimu ujao wa ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.






No comments