WATU 5 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI HAI ( MTO KIKAFU) KILIMANJARO
Na.Vero Ignatus ,Kilimanjaro
Ajali mbaya imetokea maeneo ya daraja la kikavu wilayani Hai Kilimanjaro na kusambabisha vifo vya watu 5
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Suleiman Issa amesema kuwa ajali hiyo imesababishwa na lori la kampuni ya bonite lililokuwa limehama njia na kuelekea ilipokuwa noa iliyokuwa inatoka moshi kuelekea sanya juu.
Amesema noa hiyo ilikuwa imepakia abiria 10 waliokuwa wanaelekea sanya juu ambapo 5 kati ya abiria hao wamepotea maisha ,wanawake 2 na wanaume 3 ,wamejeruhiwa 5 na abiria wawili wa lori nao wamejeruhiwa na kufikisha idadi ya majeruhi kufikia saba.
Kutokana na ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Suleiman Issa amewataka madereva kuwa makini wawapo barabarani wakati wote haswa kipindi hichi cha mvua ili kuepuka ajali zisizo za lazima.
Aliyetambulika kati ya waliopoteza maisha ni askari polisi mwenye nambari E6511 Koplo Nassir aliyekuwa akitoa huduma katika kituo cha polisi Majengo Moshi Kilimanjaro,ambae ni kocha wa Riadha,ambapo zamani alikuwa mwanariadha wa Taifa amabe ameshiriki mbio za kimataifa nchi mbalimbali ,mpaka alipostaafu na kuwa kocha wa Riadha.
Mwingine aliyetambulika ni mke wa dereva wa noa iliyopata ajali Mrs Joyce mke wa Samwel Mzava,kabila mnyaturu 50, waliopoteza Yunice Peter miaka 45 mkazi wa bomang'ombe,wawili bado hayajatambulika ,jeshi la polisi linafanya jitihada ili kuyafahamu.
Majina ya majeruhi 1.Tetropia Assenga mchanga miaka 45 Samwel Mzava 61 mpare mkazi wa bomang'ombe ,Loveness Mbise 35 Mmeru mkazi wa King'ori ,Monica Mbise Mmeru 35-40 mmeru mkazi wa king'ori,Petronila Tarimo mwanafunzi wa sekondari Rombo Mkuu
Majeruhi wawili ambao hawaongei hawatambulikani ni wawapi wamelazwa hospitali ya KCMC .


No comments