*TANZIA * Mmwanariadha Ismail Juma afariki kwa ajali -Manyara

Mwanariadha  Ismail Juma Gallet enzi za uhai wake.

Na.Vero Ignatus.

Mwanariadha aliyevunja rekodi ya Taifa kwa kukimbi dakika 59 sekunde 30 katika mbio za nusu Marathon ambazo ni kilometa 21mwezi uliopita Ismail Juma Gallet amefariki kwa  ajali ya pikipiki .

Akithibitisha kutokea kwa msiba huo Katibu mkuu wa Riadha nchini Wilhelm F.Gidabuday amesema kuwa ajali hiyo imetokea kijiji cha Gendi wilaya ya Babati mkoa wa Manyara majira ya saa kumi jioni ambapo pikipiki iligongana uso kwa uso na fuso na kusababisha kifo chake.

Leo majira ya saa kumi jioni Mwanariadha *Ismail Juma Gallet* amepata ajali ya hapo Kijijini kwao *Gendi Wilaya ya Babati - Mkoa wa Manyara ,pikipiki kugongana uso kwa uso na Fusso na kufariki papo "alisema

Mwezi uliopita Ismail alivunja rekodi ya taifa kwa kukimbia *dakika 59 sekunde 30 katika mbio za Nusu Marathon ambazo ni 21 Kilometa,ambapo Marehemu Ismail Juma alikuwa kati ya wanariadha ambao majina yao yameshawasilishwa ofisi za TOC tayari kwa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Madola (2018 Gold Coast Commonwealth Games).

"Huu ni msiba wa Taifa, alikuwa aende kuitetea Tanzania kwa kusaka medali na kupeperusha bendera ya taifa; lakini Mungu amemwita mapema"

Tunasubiri taratibu zingine kutoka kwa familia ya wafiwa. Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya *Murara* Babati.

Kwa niaba ya Chama cha Riadha Tanzania natoa pole kwa familia yake, tunakiri kupata pengo ambalo halitazibika.

*Habari hizi zimethibitishwa na;
1) Mzazi wa Marehemu
2) Uongozi wa Riadha Manyara*


No comments