Uchaguzi Kenya2017: Rais Uhuru Kenyatta aapishwa

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi siku ambayo rais Uhuru Kenyatta ameapishwa rasmi kuwa rais kwa awamu ya pili
Kenyatta na Ruto wafunga sherehe kwa maombi
Rais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto wamekamilisha sherehe za leo uwanja wa Kasarani kwa maombi, Bw Kenyatta ameongoza kwa Kiingereza na Bw Ruto kwa Kiswahili.
Baadaye, wimbo wa Jumuiya ya EAC umechezwa na kisha wimbo wa taifa la Kenya kuhitimisha sherehe za leo.
Wageni wameanza kuondoka uwanjani, wakianza na viongozi wa nchi.
Kenyatta awahimiza Wakenya kuishi kama majirani
Kwa mara nyingine, Bw Kenyatta amewahimiza Wakenya kuishi kama majirani. Amesema majirani hufaana sana na ndio hutegemewa wakati wa shida.
Ameagiza watahiniwa wote wa darasa la nane waliofanya mtihani wao mwaka huu wawe wamefahamu shule za sekondari watakazojiunga nazo kabla ya Krismasi
No comments