Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani ,Sumatra waendesha zoezi la ukaguzi wa Magari ya kusafirishia abiria Arusha.
Na.Vero Ignatus Arusha
Jeshi la polishi kitengo cha usalama barabarani Arusha kwa kushirikiana Sumatra na wadau wengine wameendesha zoezi la ukaguzi wa magari ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani Jijiji Arusha pamoja na kukagua uimara wa magari,mikanda,kuwapima Ulevi madereva wa vyombo vya usafiri kabla ya kuanza safari.
Mrakibu wa Polisi Joseph Charles Bukombe Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha amesema kuwa operesheni hiyo ni maalumu kwaajili kuhakikisha kuwa sheria zote za usalama barabarani zinafuatwa na ratiba zilizowekwa na Sumatra kama zinafuatwa
"Tumebaini kuwa yapo magari yanayosainiwa saa 12:00 asubuhi na anatakiwa atoke saa 7:00 lakini kwa kujiamulia wao wanaondoka saa 12:00 hii tabia tutaikomesha''alisema Bukombe.
Amewataka Wamiliki watambue kuwa katika magari yao wameajiri watu 4 ambao ni dereva, kondakta,wakala pamoja na fundi ili kuhakikisha chombo kipo salama kwa safari ya wote na abiria wapo salama kwa safari
"Inasikitisha kuona pale gari linapokaguliwa linakuta mikanda yake ni mibovu,matairi ni kipara,viyu vinhi kwenye gari hilo vipo hovyo wakati wapo watumishi ndani ya gati zaidi ya wanne''alisema Bukombe
"Wamiliki pamoja na watumishi wengine wanne ndani ya gari hakikisheni kuwa, abiria wanapoingia ndani ya gari wafunge mikanda ,na madereva waache tabia mbaya waliyoizoea ya kuja stendi zikiwa zimebakia dakika chache gari liondoke
Mrakibu wa Polisi Joseph Charles Bukombe Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha akiwa katika stendi kuu ya mabasi mkoani Arusha .Picha kwa hisani ya Vero Ignatus Blog.Mmoja wa Askari wa kikosi cha Usalama barabarani Sajenti Rajabu akimpima mmoja wa Madereva katika stendi ya mabasi kabla ya kuanza safari.Picha kwa hisani ya Vero Ignatus Blog.
![]() |
Kama inavyoonekana katika picha baadhi ya askari wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Arusha wakiendesha zoezi la ukaguzi wa magari .Picha kwa hisani ya Vero Ignatus Blog.
Dereva wa Basi la Kampuni ya Mbazi Aminiel Mrema akiwa amemaliza kupimwa ulevi na mmoja wa askari wa Kikosi cha usalama barabarani leo.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.
Meneja wa Sumatra Mkoani Arusha Alen Mwandry akizungumza na waandishi wa habari.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Meneja wa Sumatra Mkoani Arusha Alen Mwandry akizungumza na waandishi wa habari.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Kwa upande wake Meneja wa Sumatra mkoani Arusha Alen Mwandry amesema wanakagua nauli elekezi kama zinafuatwa na kuhakikisha hakuna abiria anachajiwa zaidi, pia wamejipanga kuhakikisha sheria za usafirishaji zinazingatiwa,kuangalia leseni na njia halali ambayo wamiliki wameomba kupeleka vyombo vyao kwaajili ya kusafirisha abiria.
"Tumezikuta gari mbili za Bukoba wamezidisha nauli na tayari tumeshawawajishisha " alisema Mwandry
Amewataka wasafirishaji kufuata sheria haswa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo kunakuwepo na abiria wengi, Sumatra imejipanga kutoa vibali vya muda vya usafirishaji katika kipindi cha mwisho wa mwaka kuelekeza magari ya ruti nyingine katika mikoa ambayo itakuwa na uhitaji wa usafiri.
Picha ya juu askari wa kikosi cha usalama barabarani akimuandikia faini mmoja wa dereva aliyekutwa na kosa,picha ya Chini Vehicle inspector akimuelekeza abilia namna ya kugunga mkanda akiwa amekaa kwenye siti .Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.





No comments