WATU 5 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI HAI ( MTO KIKAFU) KILIMANJARO


Na.Vero Ignatus .Kilimanjaro.

Ajali mbaya imetokea leo majira ya saa tisa alasiri  maeneo ya daraja la kikavu wilayani Hai Kilimanjaro na kusambabisha vifo vya watu 5

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Suleiman Issa amesema kuwa ajali hiyo imesababishwa na lori la kampuni ya bonite lililokuwa limehama njia na kuelekea ilipokuwa noa iliyokuwa inatoka moshi kuelekea sanya juu.

Amesema noa hiyo ilikuwa imepakia abiria 10 waliokuwa wanaelekea sanya juu ambapo 5 kati ya abiria hao wamepotea maisha na watano wamejeruhiwa ,na abiria 2 wa lori nao wamejeruhiwa na kufikisha idadi ya majeruhi kufikia saba.

Kutokana na ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Suleiman Issa amewataka madereva kuwa makini wawapo barabarani wakati wote haswa kipindi hichi cha mvua ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Hadi sasa watu hao watano waliopoteza maisha majina yao bado hayajatambulika ,jeshi la polisi linafanya jitihada ili kuyafahamu.

No comments