TMF YAWAPIGA MSASA WAANDISHI MANYARA.
Mkurugenzi mkuu wa TMF Ernest Sungura akizungumza na waandishi wa habari wa Manyara na mikoa jirani katika uzinduzi wa utoaji ruzuku kati ya TMF na Radio Habari Njema
Mshauri Mwandamizi wa Maarifa na Mafunzo kutoka Wakfu wa Vyombo vya Habari (TMF )Dastan Kamanzi akiwa anazungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya siku moja Mkoani Manyara wilaya ya Babati katika ukumbi wa hotel ya White Rose.
Sr.Lucy Sungu Mkurugenzi wa Radio Habari njema Mbulu
Padre Antony Lagwen ambae ni muhasibu mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbulu akizungumza katika uzinduzi wa mradi mpya wa TMF White Rose Babati.
Mkuu wa wilaya ya Babati Chelestino Simbulimile Mofuga akishuhudia Padre Urbano Sule makamo wa askofu jibo katoliki labulu akisaini mkataba mpya kati ya TMF na Radio habari njema
Mkurugenzi mkuu wa TMF Ernest Sungura akiwa anafuatilia Padre Antony Langwen akiweka saini ya mkataba mpya kati ya Radio Habari njema ya Mbulu na TMF.
Picha ya pamoja ya wanaandishi mbalimbali waliohudhuria mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika Hotel ya White Rose Babati.
Na.Vero Ignatus Manyara.
Wakfu wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) umeendesha mafunzo ya siku moja ya waandishi (35)wahabari mkoani Manyara yakiwa na lengo la kuwanoa wanahabari ili waweze kuandika habari kwa makini na waepuke kuandika habari za uchochezi bali waandike habari ambazo zinaleta tija kwa jamiii
Akitoa mafunzo hayo Mshauri Mwandamizi wa Maarifa na Mafunzo (TMK)Dastan Kamanzi amesema kuwa mwandishi wa habari anayejitambua lazima afanye kazi yake kwa umakini huku akitambua wajibu wake kuwa ni kulinda,kushitaki na Kushauri .
Mafunzo hayo yaliambatana uzinduzi wakutoa Ruzuku kati ya TMF na Radio habari na ikiwa ni ruzuku ya mradi mpya wa Pambazuka (4) ambao ni zaidi ya milioni 112.
Mkurugenzi mkuu wa TMF Ernest Sungura amesema kuwa Radio hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika miradi mingine iliyopita katika ameitaka radio hiyo katika mradi huo mpya wawekeze zaidi katika utafiti na kukidhi matakwa ya walaji wao na kubuni mbinu za mabadiliko,kuwabadilisha fikra ,wawe na mbinu mbalimbali za kutafuta pesa,kibiashara,kimkakati na kiuongozi.
Kwa hupande wake mkuu wa wilaya ya babati Chelestino Simbulimile Mofuga amewataka waandishi wa habari kuwa makini na wazalendo,wasiandike habari za uchochezi ambazo zitahatarisha Amani ya nchi.
"Yatumieni mafunzo mliyopewa vizuri kuandika taarifa zisizokuwa za uchochezi'alisema mkuu huyo wa wilaya.
Ikumbikwe kuwa Radio ya habari njema imeshawahi kuchukua ruzuku awamu 3 ukiwemo ule wa mwaka 2012 milioni 42,kwaajili ya mradi wa Wanawake tuzungumze,2014 milioni 50 wanawake tuzungumze awamu ya pili ,2016-2017 milioni 60 kwaajili ya kuhamasisha elimu ya vyoo na maji kwa mkoa wa Manyara.
.








No comments