WANAFUNZI ZAIDI YA 300 WAPATA ELIMU KUHUSU ELIMU YA MMEA HATARISHI WA GUGU KAROTI

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Lemara katika Jiji la Arusha wakiwa tayari kwaajili ya kupatiwa elimu kuhusu mmea hatarishi wa gugu karoti.
Muwezeshaji Anna Sanare kutoka Taasisi ya( ECHO)nchini akizingumza na wanafunzi katika shule ya msingi Lemara iliyopo katika Jiji la Arusha kuhusiana na mmea hararishi wa gugu karoti.
Charles Bonaventure mtaalamu wa gugu karoti kutoka Taasisi ya (ECHO)aliyeshika bango akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lemara iloyopo Jiji la Arusha,kushoto kwake ni Mtaalam kutoka Taasisi ya Peace Corps Tanzania Malvery Begley
Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Lemara akizungumza na wanafunzi kabla ya kuwatambulisha wageni hao shuleni hapo (hawapo pichani)picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.
Wageni wakiwa wanatambulishwa kwa wanafunzi.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.
Wanafunzi wakiwa wamenyosha vidole tayari kwa kuuliza maswali juu ya mmea hatarishi wa gugu karoti.picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.

Aliyepo nyuma mrefu ni mwalimu mkuu msaidizi akiwa pamoja na wataalamu na muwezeshaji wa gugu karoti Charles Bonaventure kutoka Taasisi ya Echo,Anna  Sirikwa Muwezeshaji ,Anita James kutoka Echo na Taasisi ya Peace Corps Tanzania Malvery Begley
Darasa likiwa linaendelea.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.
Wanafuanzi wakiwa wametulia wakisikilizabkwa makini .Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.
Mwezeshaji wa Gugu Karoti Anita James akiwa ameshika gugu karoti mkononi akiwaonyesha wanafunzi Mwezeshaji wa Gugu Karoti Anna Sirikwa na Mtaalamu wa gugu karoti Malvery Begley Corps
Mtaalam wa Taasisi ya Peace Corps Tanzania  Malvery Begley akiwa anagawa mipira ya kuvaa miononi (gloves)kwa wanafunzi kwaajili ya kung'olea gugu karoti.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.
Mmoja wa mwanafunzi akiwa anang'oa gugu karoti akiwa amevaa mpira wa plastoki mikononi.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.


Wanafunzi wakiwa wameshika gugu karoti baadabya kuyang'oa katika maeneo ya shule yao na kuyatupa jalalani tayari kwa kuyachoma.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.


Na.Vero Ignatus ,Arusha 

Taasisi ya ushauri wa Kilimo  na Mazingira ya  (ECHO) kwa kushirikiana na  Taasisi ya Peace Corps Tanzania wametoa elimu kwa wanafuzi wa shule ya msingi Lemara iliyopo Kata ya Lemara Jijini Arusha kuhusiana na mmea hatarishi wa gugu karoti


Akizungumza na wanafunzi katika shule ya msingi Lemara iliyopo kata ya Lemara katika jiji la Arusha bi Anna Sirikwa ambaye ni muwezeshaji kutoka( Echo)amesema kuwa gugu hilo lilitokea Amerika ya kati na kwa bahati mbaya limeenea katika nchi nyingi  lilianza kukua  kwa kasi mkoani Arusha kuanzia miaka ya 2010.


Amewaambia wanafunzi hao kuwa gugu hilo ni hatari kwani linapunguza kukua ,kuota kwa mazao ,ni hatari kwa afya ya binadamu na wanyama,linahatarisha maisha ya viumbe wengine,linaweza kusababisha jangwa, gugu hilo linasababisha magojwa kama vile pumu na aleji ya ngozi


Ameainisha njia ambayo ni ya kuzuia gugu hilo ni kwakuling’oa na kulichoma kabla ya kuota mbegu  ,amesema mmea huo hatarishi tunda moja linaweza kuzaa mbegu 25,000 mara tatu kwa mwaka na kufikia 75,000-90,000 na husambaa kwa haraka sana.

No comments