JESHI LA POLISI WAENDESHA ZOEZI LA UKAGUZI WA MAGARI MKOANI ARUSHA

Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani (ASP )Joseph Bukombe akiwa anakagua moja ya basi kabla halijaanza safari ,ambapo pia aliweza kuzungumza na abiria kuhusiana na usalama wao wawapo safarini.Picha na Vero Ignatus Blog.


Muonekanao wa Stend ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani Jijini Arusha kama inavyoonekana .Picha na Vero Ignatus Blog


 Askari wa kikosi cha usalama barabarani Jijini Arusha wakiendelea na ukaguzi wa magari kama wanavyoonekana Pichani.Picha na Vero Ignatus Blog.
Ukaguzi ukiendelea sambamba na ulipaji wa faini kwa magari yaliyopatikana na makosa.Picha na Vero Ignatus Blog.
Pilikapilika zikiendelea katika stendi hiyo ya mabasi Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.


Mmoja wa dereva akipewa maelekezo na askari katika stendi kuu ya mabasi baada ya gari lake kukaguliwa .Pixha na Vero Ignatus blog.
Ukaguzi ukiendelea stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya Askari wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha wakiwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapo Joseph Bukombe( aliyeshika fimbo) katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kazi ukaguzi wa magari katika stendi kuu ya mabasi yaendayao mikoani na nchi jirani Jijini Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog

Na ,Veo Ignatus  Arusha.





Ukaguzi wa magari yanayobeba abiria( haice ,mabasi )unaendelea katika jiji la Arusha ambapo ukaguzi unafanyika kuangalia uimara wa mikanda ndani ya magari,matairi,pamoja na mambo yote muhimu katika vyombo hivyo huku zoezi  hilo likienda sambamba na maandalizi ya  wiki ya nenda kwa usalama barabrani mkoani hapo

Mrakibu wa polisi Joseph Bukombe ambae ni mkuu wa kikosi cha usalama barabrani mkoa wa Arusha amesema kuwa  zoezi hilo ni endelevu kwani ili kuwajengea Watanzania elimu na uwezo pale watakapoingia kwenye mabasi ya abiria wahakikishe kuwa wanafunga mikanda ,itakapofika mwaka 2020 walau kila familia iwe na uelewa juu ya ufungaji mikanda na wasisubirie hadi wasimamiwe na askari.

 "Tuondokane na hii tabia ya watanzania ili aweze kufunga mkanda lazima asimamiwe na askari"alisema Bukombe.

Amesema jeshi la polisi wanaendelea kutoa Elimu hiyo hadi pale watakapoona wananchi wanabadilika ili waweze kufikia malengo,amesema ni vigumu kufikia Tanzania ya viwanda kama nchi itapoteza nguvu kazi au kuwa na majeruhi vilema ambao hawafanyi kazi kutokana na ajali za barabarani kwani maendeleo yeyote lazima yawe na nguvu kazi.

Amewataka madereva wote wanapokabidhiwa vyombo vyao vya moto  hususani vya abiria kuwa makini kabla hawajaanza safari wakague magari yao ili waweze kutambua kama kuna tatizo lolote ambalo linaweza kuleta madhara kwa binadamu wanapokuwa  safarini 

Ameitaja kauli ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ni Endesha salama Tii sheria,Okoa maisha .Ikumbukwe kuwa wiki ya nenda kwa usalama barabarani Kitaifa ilifanyika hivi karibuni   Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro katika Uwanja wa mashujaa 










No comments