WATANZANIA TUACHE UWOGA KILIMO CHA NYUMBA YA KIJANI KINALIPA.
Mkurugenzi wa Wigo Farming Production Godson Moshi akionyesha akionyesha mche wa Hoho ukiwa katika hatua za awali za kutoa matunda,ambapo unaonekana ukiwa tayari na matunda sita ambapo kila mche unauwezo wa kutoa matunda kwa kila wiki.
Aina ya nyanya iitwayo Cherry tomato ambayo wengi wamezowea kuiita (nyanya pori ) ikiwa imezaa vizuri tayari pia imeanzwa kuvunwa ,mche wake unarefuka hadi urefu wa mita 10.Mbegu yake kwa kitaalam inafahamika kama FORTESA ambapo tawi moja linatoa nyanya 18-35.
Aina ya pilipili hoho ambayo pilipili za rangi ,inaanza kuwa Kijani,inaendelea kubadilika na kuwa Zambarao, baadae inakuwa Nyekundu ambapo mbegu zake zinafahamika kitaalam kama PASARELLA,Pilipili hizi ni nzuri sana kwa juice ,kupika inavirutubisho vya kutosha kwaajili ya mwili wa binaadamu.
Ndugu Godson Moshi akionyesha hoho.ya njano.inavyoonekana ikiwa imeshabadilika rangi kutoka kijani kuwa ya Njano ,ikiww tayari kwa kuvunwa kupelekwa sokoni.
Cherry tomato ikiwa inaonekana jinsi linavyozaa kwa wingi ambapo tawi moja linauwezo wa kuzaa nyanya kuanzia 18-35 huku mche mmoja unauwezo wa kutoa kilo 20-30 za nyanya.
Pilipili hoho ikiwa katika muonekano tayari imeshaanza kubadilika rangi,kama inavyoonekana,Itaendelea kubadilika yote hadi kuwa na rangi moja ya Njano.

Hoho nyekundu zikiwa zimevunwa tayari kwa kwenda sokoni hizi zinabadilika kutoka Kijani na kubadilika rangi kuingia nyekundu.
Pilipili hoho za rangi inavyobadilika kutoka rangi ya Kijani ,Zambarau na kuingia rangi nyekundu kama inavyoonekana kwenye picha.
Mkurugenzi wa Wigo Farming Production akionyesha nyanya mshumaa,ambapo aina hii ya nyanya inalimwa kutokana na mahitaji ya soko kwani watu wengi wanazipenda kutokana siyo chachu na zina ladha nzuri kwenye chakula, pia ndiyo nyanya iliyopo kwenye soko kwa sasa.Mche wa nyanya hii unarefuka hadi kufikia mita 10,kwa wiki unaweza kuvuna kilo 1-1.5.
Ndugu Salum Sefu akiwa anavuna hoho ambazo zimekishawiva tayari ,kuzivuna lazima uwe na utaalamu ili usiharibu tawi na ili ziweze kuendelea kuzaa vizuri pia hizi nazo zinarefuka hadi urefu wa mita 10.
Ndugu Salum Sefu akiwa tayari ameshavuna hoho,anaziandaa kwa kupelekwa sokoni.
Na.Vero Ignatus, Arusha.
Wito umetolewa kwa serikali iwasaidie wakulima kuondokana na kilimo cha wazi,watumie kilimo cha (Green house)nyumba ya kijani ili waweze kujikwamua kutoka kwenye kilimo cha umaskini ambacho wanatumia gharama kubwa na nguvu nyingi .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa Wigo Farming Production iliyopo jijini Arusha, ya kwamba mkulima anapotumia kilimo cha Nyumba ya Kijani( green house)inamsaidia mkulima kuuza mazao yake kwa usahihi na kwa uhakika maana atakuwa ametumia kilimo ambacho kinatumia mbolea za asili zisizokuwa na kemikali.
Amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa (Green House)gharama zake na vifaa ni ghali, upatikanaji wa mbolea za asili kama vile mkojo wa Sungura ambao inawalazimu kuuagiza kutoka Nchi jirani ya Kenya, Mkojo wa ng'ombe ,kwani kilimo hiki hakitumii mbolea za kawaida.
Aidha ameongeza kuwa kama wakulima watasaidiwa nakupewa elimu ya kutosha kuhusu kilimo cha Nyumba ya Kijani, kitamuingizia mkulima faida mara kwa mara kwani kwa sasa soko ni kubwa lakini bidhaa zinazohitajika ni watu wachache tu ndiyo wanalima.
"Kwa mkulima anayelima kilimo hichi cha (Green house)gharama zake ataziona pale awali wakati anaandaa nyumba ya kijani,lakini baada ya muda mfupi sana mkulima huyu ataanza kuona faida na gharama zake zote zitarudi bila usumbufu wowote,hata kama umechukua mkopo utaulipa kwa wakati maana kilimo hichi kinalipa,pia masoko ya kuuza mazao yapo haswa nchi za Uarabuni na Ulaya pamoj na.kwenye mahoteli makubwa ya Kitalii, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu tuingie tuanze kulima ,tuondoe woga"Alisema Godson Moshi.





No comments