UZINDUZI WA MBIO ZA WEST KILI FOREST TOUR 2024 WAFANYIKA SIHA KILIMANJARO

b
 Mkuu wa wilaya wa wilaya ya Siha Dkt.  Christopher Timbuka,akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika eneo la msitu wa West Kilimanjaro uliopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
PCO Robert Faida ni Mkuu wa Hifadhi shamba la miti West Kilimanjaro akizungumza na kutoa ufafanuzi juu ya mbio zitakazofanyika juni 2024
Afisa Uhusiano TFS Johari Kachwamba ambaye alimuwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Prof. Dos Santos Silayo akizungumza katika uzinduzi wa mbio za West Kili forest tour challange 2024 umezinduliwa rasmi leo na   ya nne 
Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa makampuni wazawa TLTO Samuel Daniel Diah 
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Siha Dkt.  Christopher Timbuka,akiwa pamoja na PCO Robert Faida Mkuu wa Hifadhi shamba la miti West Kilimanjaro wakitembelea baadhi ya maeneo ya vivutio kama scheme ya uzinduzi rasmi wa mbio za West Kili forest tour challange 2024
Baadhi ya Waendesha baiskeli na waendesha pikipiki wakiwa katika siku ya uzinduzi wa mbio za West Kili forest tour challange 2024 wilaya  ya Siha Mkoani Kilimanjaro. 
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Siha Dkt.  Christopher Timbuka,akiwa pamoja na PCO Robert Faida Mkuu wa Hifadhi shamba la miti West Kilimanjaro wakitembelea baadhi ya maeneo ya vivutio kama scheme ya uzinduzi rasmi wa mbio za West Kili forest tour challange 2024

UZINDUZI WA MBIO ZA WEST KILI FOREST TOUR WAFANYIKA SIHA KILIMANJARO

Na. Vero Ignatus,Kilimanjaro

Msimu wa Mbio za msituni maarufu kama West kili forest tour challange 2024 umezinduliwa rasmi  mei 23 na Mkuu wa wilaya ya Siha Dkt Christopher Timbuka,uzinduzi uliofanyika katika eneo la msitu wa West Kilimanjaro uliopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Dkt.aliwaambia waandishi wa habari kuwa Zaidi ya washiriki 500 wanataraji kushiriki mbio hizo ambazo pia zitashirikisha mashindano ya baiskeli na pikipiki.ambapo mbio hizo zinalenga kukuza utalii endelevu kuhamasisha uhifadhi pampja na kuwaleta wageni na wadau mbalimbali kujifunza na kushirikiana kwa manufaa ya jamii na mazingira kwa ujumla.

PCO Robert Faida ni Mkuu wa Hifadhi shamba la miti West Kilimanjaro amewaambia waandishi wa habari Jana mei 23/5/2024 kwamba shindano hilo la nne linatarajiwa kuwa na wageni zaidi ya 500 ambapo likiazishwa  rasmi tarehe 22/6 2021 likiwa na washiriki wapatao 200 kutoka ndani na nje ya nchi, 22-2023 washiriki waliongezeka hadi kufikia 300 sawa na wastani wa asilimia 40

PCO Robert amesema kuwa mashindano hayo yana tofauti kubwa na mbio nyingi new kwani washiriki watakimbia maeneo yaliyojaa Utajiri wa Bioanuai na vivutio vingi vya Kiekolojia, hivyo wanawakaribisha wawekezaji, wa day mbalimbali pamoja na wadhamini zaidi katika shughuli hiyo. 

"Hadi sasa Mataifa ambayo yamethibitisha ushirikiano wait katika mbio hizo ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Congo, Polland, Ufaransa na Uingereza, tunawakaribisha wawekezaji, wadau mbalimbali na wadhamini zaidi wajitokeze katika kudhamini shughuli hii". Alisema 

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa makampuni wazawa TLTO Samuel Daniel Diah amewashauri waandaaji wa West kili ifike wakati wafanye maamuzi ya kuamua kuyaita mashindano hayo kuwa kimataifa kwasababi idadi ya washiriki kila make kitoka nje ya nchi wanekuwa wakiongezeka 

"Lego la Mashindano haya ni kutangaza utalii na vivutio vyake basi ifike mahali sasa kufanya tukio hili kuwa la kimataifa zaidi kutoka na na wage ni mbalimbali wanapshiriki. Sisi ni wwtumiaji wa mazao ya TFS kwa. Mfano tunapopanda milima tu napita katika maeneo ya TFS safari za siku kwenue maporomoko ya maji napuri yote hayo tinayauza kwa wageni wetu" 

Aidha mbio hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 21-23 juni ,2024 ambapo kutakuwa na matembezi ya riadha na utalii ambapo wageni watachagua umbali tofauti tofauti kilometa 21,10,na km5 huku wakifurahia madhari mazuri yenye vivutio vya asili.

Sambamba na hilo washiriki wa michezo wa pikipiki watalipa ada ya ushiriki shilingi za kitanzania 30,000,watakaoshiriki mbio watatakiwa kulipa ada ya sh 35,000 na wabobezi pro riders watalipa pesa za kitanzania shilingi 65,000.


No comments