RC MAKONDA ASISITIZA VIJANA KUWA NA UTHUBUTU NA KUJIAMINI
RC MAKONDA ASISITIZA VIJANA KUWA NA UTHUBUTU NA KUJIAMINI
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka vijana kujiamini na kuwa na uthubutu katika kupambana kwenye kuzifuata ndoto zao na malengo waliyojiwekea kwenye maisha yao.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo leo Mei 29, 2024 wakati akizungumza na vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Arumeru mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arumeru alipokuwa akianza ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mhe. Mkuu wa mkoa amewataka vijana kutokuogopa watu wanaowashangaa ama kuwaona kutokuwa sawa kiakili wakati wanapopambana kuhakikisha wanatimiza kile wanachokiamini akitolea mfano wagunduzi wa huduma na vitu mbalimbali ambavyo havikuwa rahisi kubaini ikiwa vingeweza kufanya kazi kama ambavyo vinafanya kazi hivi sasa.
Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa mkoa amewataka vijana kuwa waadilifu na kuikataa rushwa kwenye maeneo yao hasa wakati wa uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka 2025 na ule wa serikali za mitaa utakaofanyika baadae mwaka huu.
No comments