RC MAKONDA ATOA WANASHERIA KUSIMAMIA KESI YA MTOTO ALIYEBAKWA TENGERU
RC MAKONDA ATOA WANASHERIA KUSIMAMIA KESI YA MTOTO ALIYEBAKWA TENGERU
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameahidi kutoa wanasheria kutoka Chama cha Wanasheria wa Tanganyika Kanda ya Arusha TLS kumsaidia Mama aliyejitokeza kwenye mkutano wake wa Hadhara na kueleza kuhusu tukio la mjukuu wake wa kike kubakwa tangu Novemba mwaka jana na kushindwa kuendelea na kesi kutokana na kukosa fedha ya kumlipa wakili wa kusimamia kesi hiyo.
Kulingana na Bibi huyo (kwenye video) amemuambia Mkuu wa Mkoa kuwa mjukuu wake alibakwa na Kijana anayedaiwa kubaka watoto wengine wanne eneo la Tengeru na Polisi wameshindwa kumkamata kwa muda mrefu sasa.
Akizungumzia siku ya tukio amesema Novemba 5, 2023 alipata ugeni na baadae akamtuma mjukuu wake huyo kwenda kumtafutia mgeni pikipiki (bodaboda) na wakati mtoto huyo akiwa njiani ndipo Mtuhumiwa alipomuita chumbani kwake na baadae kumfanyia vitendo vya kikatili.
Mama huyo amemuambia Mkuu wa Mkoa kuwa kutokana na mtuhumiwa kuwa na fedha, kesi dhidi yake ilimalizika kwa namna ambayo hakuridhika nayo baada ya mahakama kudai kuwa hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha mtoto huyo kubakwa na mtuhumiwa husika.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ameonesha kusikitishwa na taarifa hiyo akihoji namna ambavyo Mahakama ilishindwa kutumia ushahidi wa daktari ambaye alimpima mtoto huyo na baadae kumuanzishia dozi za kuzuia maambukizi.
Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru kumsaka na kumkamata mtuhumiwa huyo kabla ya siku ya kesho na kuanza taratibu za kumfikisha mahakamani.
No comments