Rais Magufuli azindua magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua ghala ya dawa kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison na viongozi wengine.
Sehemu ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) yaliyozinduliwa jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund, Bw. Linden Morrison wakati akijaribu moja ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua sehemu ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund, Bw. Linden Morrison na viongozi wengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia
kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.
Sehemu ya wafanyakazi wa MSD wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison wakati akijaribu moja ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe
kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018. Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison akijaribu moja ya magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.
PALE WAPIGA PICHA WANAPOPIGWA PICHA - Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiupiga picha msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison (chini kushoto) na viongozi wengine wakati wakielekea kukagua magari 181 ya Bohari kuu ya Madawa (MSD) aliyozindua jijini Dar es salaam leo Machi 26, 2018.
Picha na IKULU
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwaambia viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuwa wasikubali kuwa vilaza baada ya kugundua Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA imekuwa kikwazo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Rais Magufuli amesema hayo leo Machi 26, 2018 wakati akizundua magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ambayo yanategemewa kuanza kusafirisha dawa mijini na vijinini
Akiwa kwenye uzinduzi huo Rais Magufuli alipokea malalamiko kuwa zipo baadhi ya taasisi za serikali zimekuwa zikichangia kukwamisha ucheleweshwaji wa dawa ambazo zinaletwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
"Nimesikia saa zingine kunakuwa na ucheleweshwaji kati ya taasisi fulani fulani ndani ya serikali taasisi ya vyakula TFDA, mnaleta madawa halafu mnashindwa kupata kibali bandarini, madawa yanacheleweshwa inawezekana 'expire date' yake inafika madawa bado yamezuiliwa pale bandarini.
" Mimi atakae zuia madawa haya niambieni ili nijue chombo gani cha serikali, niambieni tu huyo aliyezuia nione ili na mimi nimzuie yeye moja kwa moja,kuna mambo mengine ni rahisi sana wala msilalamike bali mwambie Waziri au Katibu Mkuu" alisema Rais Magufuli
Magufuli aliendelea kuweka wazi kuwa watu ambao wanakwamisha na kuchelewesha dawa kutoka ni watu ambao pia wanatoka katika wizara hiyo hiyo wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
"Hata aliyempa nguvu ya kuzuia dawa wapo chini ya wizara yenu yaani ni nyinyi wenyewe, basi nyinyi vilaza sasa mtu yupo chini yenu, yaani mtu anayezuia yupo kwako anayezuiliwa yupo kwako bado mnakaa mnaimba nini.
"Mimi nataka haya niyashughulikie unajua mambo mengine mnakwamishana nyinyi wenyewe kama ni TRA mwambie Katibu Mkuu, mwambie Waziri wa Afya, mwambie Waziri wa Fedha tufike mahali tusikwamishane, kwa sababu anaweza akawa amekwamisha madawa yenu lakini madawa ya mtu binafsi anayaruhusu siku hiyo hiyo sasa hili ni lenu wala halihitaji kufika kwangu" alisisitiza Magufuli








No comments