Wanandoa wafa maji Ngorongoro huku mtoto wao akinusurika Kifo
Miili ya watu wawili ambao ni wanandoa imeokotwa baada ya kuchukuliwa na mafuriko katika mto Piyaya Kata ya Piyaya wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo amesema miili hiyo imeonekana leo majira ya asubuhi baada ya maji ya mto huo wa msimu kupungua.
Ameyataja majina na wanandoa hao waliokufa maji kuwa ni Ormins Sunguyo na mkewe Nembris Sunguyo ambao walikuwa na mtoto wa mdogo aliyefahamika kwa jina la Oloosukuta Sunguyo ambaye alinusurika kifo.
Kamanda Ilembo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi katika mkoa wa Arusha kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua na kuepuka kuvuka mito wakati maji yanafurika.
No comments