MGOGORO WA MIPAKA KIMOTOROK WACHUKUA SURA MPYAr

 Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa manyara Alexander Mnyeti akiwa sambamba na waatalam mbali mbali wa Serikali wakati akitazama alama za mipaka  iliyoweka na hifadhi ya taifa  ya Tarangire na pori la hifadhi mkungunero katika  Kijiji cha kimotoroki Wilaya ya Simanjiro mkoan manyara.

Simanjiro-Manyara

Mgogoro wa ardhi kati ya pori  tengefu la mkungunero hifadhi ya tarangire na wakazi wa kijiji cha kimotorok wilaya ya simanjiro umechukua sura mpya baada ya kamti ya ulinzi na usalama ya mkoa wa manyara kufika katika eneo ilo na kutoa siku kumi kwa wataalam wa ardhi kuhakiki upya alama za mipaka.

Baada ya kufika katika eneo ilo kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa manyara ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Manyara Elaxander Mnyeti  ilikagua mipaka  na kupata maelezo kutoka kwa wananchi  kisha ikatoa agizo ilo  la kuwataka wananchi kutokuandoka katika eneo mpaka uhakiki wa mipaka utakapofanyika upya kutoka idara ya ardhi ambalo katibu tawala msaidizi mundombinu  wa mkoa huo bi suma tukampele mwakasitu anaahidi kuyatekeleza kwa umakini mkubwa maagizo hayo.
    
kwa upande wao wakazi wa kijiji  cha kimotorok  walipata nafasi ya kutoa madukuduku yao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Manyara wanasema hawawezi kuondoka katika eneo kwani wamekaa tangu mwaka sabini na mbili na mipaka ya hifadhi ya tarangire wanaijua lakini wanshangaa kwanii wameongeza mipaka hyo huku mbunge  wa simanjiro james  ole milya akiwataka wataalamu hao kufanya uhakiki bila kupendelea upande wowote.
     
Wanachi wa kijiji cha kimotorok Wilaya ya Simanjiro  wakati wakisikiliza mkuu wa Mkoa wa manyara Alexander mnyeti Mara baada ya kukagua alama zilizowekwa na hifadhi ya Tarangire na pori Tengeru la mkungunero ktk Kijiji chao

No comments