DKT.MWAKYEMBE AWAAMSHA USINGIZINI MAAFISA HABARI NCHINI
Waziri wa Habari sanaa,Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutank wa Maafisa mawasiliano,wa serikali katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi .
Msemaji mkuu wa serikali Dkt.Hassan Abbas akizungumza katika mkutano huo .
Na.Vero Ignatus Arusha.
Dkt.Mwakyembe ametoa agizo kwa maafisa habari wote nchini watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria na malengo waliyojiwekea kwa wakati.
Agizo hilo amelitoa Kikao cha 14 cha Kazi kwa Maafisa habari ,Mawasiliano,na Uhusiano Serikalini ambacho amekifungua leo Jijini Arusha .
Dkt.Mwakyembe amesema kuwa hadi sasa Halmashauri zinazofanya vizuri katika kutoa taarifa kwa wananchi 9 sambamba na mikoa 18 tu kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Amesema Serikali haitawavumilia maafisa habari ambao hawafanyi kazi ,kwani hawana tofauti na waofisa habari hewa wanageuza tovuti za Serikali kuwa magofu badala ya kuwa na habari mbalimbali zenye tija na maendeleo kwa taifa la Tanzania.
"Msipofanya kazi kuhabarisha jamii,mnakuwa maafisa habari hewa,na haustahili ujira wowote kwani umeamua kubweteka tu." Alisema Mwakyembe.
Kwa upande wake muwakilishi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez amesisitiza maafisa hao kutumia mitandao ya kijamii kwa maslahi mapana ya taifa ili kuweza kuongeza chachu ya maendeleo kuelekea tanzania ya viwanda.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari,mawasiliano na uhusiano serikalini amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuwajengea uwezo maafisa habari,ili waweze kutekeleza majukumu yao.kwa wakati.

No comments