Walowezi wa Israel katika ukingo wa magharibi wauona ushindi wa Trump kama fursa
Walowezi wa Israel katika ukingo wa magharibi wauona ushindi wa Trump kama fursa

Chanzo cha picha,EPA
Katika siku ambayo hali ya anga iko sawa, majumba marefu yaliyopo Jijini Tel Aviv yanaonekana vizuri kutoka kwa mlima uliojuu ya Karnei Shomron, ambapo ni makazi ya walowezi wa Israel katika eneo lililokaliwa la Ukingo wa magharibi.
“Ninahisi tofauti kati ya hapa na Tel Aviv,” amesema Sondra Boras, ambaye ameishi katika mtaa wa Karnei Shomron kwa takriban miaka 40. “Ninaishi katika eneo ambalo mababu zangu wa zamani waliishi kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Siishi katika eneo lililokaliwa; Ninaishi katika eneo lililotambuliwa katika bibilia la Judea na Samaria.”
Kwa walowezi wengi wanaoishi hapa, hawatofautishi kati ya taifa la Israel nae neo ambalo taifa hilo ilinyakua kutoka Jordan katika vita vya mashariki ya kati vya 1967.
Suala hili limefutika kutoka kwenye mtazamo na matamshi yao.
Kulingana na malelezo ya wageni yaliyorekodiwa katika eneo la juu la mlimani, linaelezea ukingo wa magharibi kama eneo ambalo lipo chini ya himaya ya Israel, na kwamba mji wa Kipalestina wa Nablus, ni eneo ambalo Mwenyezi Mungu aliwaahidi wa Israeli kuwa ardhi yao.
Ila, kukatwa rasmi kwa eneo hili kumesalia kuwa ndoto kwa sasa kwa walowezi kama Sondra, japo makazi ya walowezi, yanatajwa kama makazi haramu na mahakama ya juu kabisa ya umoja wa mataifa na vilevile baadhi ya mataifa duniani, yamezidi kuongezeka mwaka baada ya mwaka.
Sasa wengi wanaona fursa ya kuendelea mbele, kufuatia uchaguzi wa Donald Trump kama Rais wa Marekani. “ Nilifurahi sana kwamba Trump alishinda uchaguzi wa Urais,” Sondra aliiambia BBC.
Ningependa sana kupanua Utaifa wa Judea na Samaria. Na ninahisi, kwamba ni jambo ambalo Trump ataliunga mkono.
Kuna ishara kwamba baadhi katika serikali ya Trump inayoingia madarakani huenda wakakubaliana na Sondra.
Mike Huckabee, ambaye ameteuliwa kuhudumu kama Balozi wa Marekani nchini Israel, ameashiria kwamba anaunga mkono madai ya Israel kuhusu Ukingo wa Magharibi katika mahojiano yaliyofanyika mwaka jana.
“Wakati watu wanatumia neno ‘KUKALIWA”, ninasema : “Ndio, Israel inakalia ardhi hiyo, lakini ni hali ya kukalia ardhi ambayo Mwenyezi Mungu mwenyewe aliwapa miaka 3500 iliyopita. Ni ardhi yao, “Alisema
Chanzo BBC
No comments