RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE KITAIFA JIJINI ARUSHA.
RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE KITAIFA JIJINI ARUSHA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo Kitaifa maadhimisho yanatarajiwa kufanyika Jijini Arusha, tarehe nane mwezi Machi 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amebainisha hayo leo Ijumaa Januari 24, 2025 wakati akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Jijini Arusha, akisema maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali kwa siku nne mfululizo, ikiwemo maonesho ya kibiashara, Michezo mbalimbali kwa wanawake pamoja na burudani zikazoambatana na nyama Choma za Ng'ombe zaidi ya mia tano.
Ametumia fursa hiyo pia kuwataka wanawake wa Mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazoambatana na maadhimisho hayo, akiwaalika wanawake kufika kwenye Ofisi za Wakuu wa Wilaya kwaajili ya kuwasilisha mawazo yao mbalimbali yatakayowasaidia kuweza kunufaika na Uenyeji wa Arusha kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake Kitaifa.
Mhe. Makonda amesema tayari Mkoa umeanza maandalizi ya Maadhimisho hayo, akiisihi jamii ya Mkoa wa Arusha kwa maana ya mtu mmoja mmoja pia kujiandaa, kwani kutakuwa na utoaji wa zawadi maalum kwa wanawake/ akinamama, zawadi ambazo zitatolewa na Watu mbalimbali kwa Wazazi wao kama sehemu ya shukrani kwa malezi.
No comments