Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Marais wa Nchi za Afrika, Wakuu wa Taasisi mbalimbali duniani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala ya Nishati katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) tarehe 28 Januari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati tarehe 28 Januari, 2025.
“Kupitia mpango huu tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko, Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha umeme Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na hivyo kuwezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Misri, tayari tumeunganisha miundombinu ya umeme na Nchi za Burundi, Kenya na Rwanda na sasa tunaendelea kuunganisha miundombinu ya umeme na Nchi ya Zambia na Uganda”
“Kuwepo kwa miundombinu hiyo kutawezesha biashara ya nishati kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme ikizingatiwa kuwa hadi November 2024 mahitaji ya umeme Tanzania yalikuwa megawatt 1888 wakati uzalishaji wetu mi megawatt 3431”
“Muelekeo wetu ni kufikisha umeme katika vitongoji vyote 64359 baada ya kufanikiwa katika vijiji vyote vya Tanzania, hadi sasa tumevifikia vitongoji 32827 na kazi inaendelea katika vitongoji vilivyobakia , la nne ambalo mpango huu utafanya ni kusambaza nishati safi ya kupikia” Rais Samia akiongea kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika leo January 28,2025 Jijini Dar es salaam.
No comments