Mitambo ya Bilioni 1.7 yazinduliwa Jijini Arusha
Mitambo ya Bilioni 1.7 yazinduliwa Jijini Arusha
Na. Vero Ignatus, Arusha
Hafla ya uzinduzi wa malori mapya na mtambo mpya wa kutengeneza miundombinu ya barabara imefanyika Leo katika uwanja wa gymcana Jijini Arusha ambao inatahamani ya shilingi za Ki Tanzania Bilioni 1.7 ambapo itatumika kukarabati miundombinu katika barabara za pembezoni
Arusha
Mhe. Meya alisema Arusha ni Jiji la kitalii hivyo amewasihi viongozi kuwahamasisha wananchi kupanda miti kwani kila halmashauri imepewa kama vile walivyopewa jukumu la kuhakikisha linapanda miti Mil1 yote hayo ikiwa ni kuhakikisha kuwa Arusha inakuwa ya kijani.
"Hamasisheni wananchi kuhakikisha mnatunza mazingira vile vile hakikisheni kuwa hawatupi chupa za plastiki pembezoni mwa barabara kwenye daladala, mabasi ya abiria ili wazingatie usafi na Jiji like safi" Alisema
Arusha
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo amesema mitambo hiyo imekuja ikiwa ni hatua muhimu ya kumaliza changamoto ya barabara mbovu katika maeneo mengi ya jiji hilo
Akisoma ripoti fupi mbele ya ngeni rasmi ya ununuzi wa mitambo hiyo Mhandisi wa Jiji la Arusha Jacobo Mwakyambiki amesema mitambo hiyo inathamani ya bil. 1.7 Lego likiwa nikukarabati miundombinu Jiji la Arusha

No comments