JESHI LA POLISI LASHIKILIA WATU 3 KWA MAUAJI YA MTOTO ARUSHA
JESHI LA POLISI LASHIKILIA WATU 3 KWA MAUAJI YA MTOTO ARUSHA
Na. Vero Ignatus, Arusha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Jaina Mchomvu, kwa tukio la mauaji ya mtoto aitwaye Mariam Juma (12) mkazi wa kwa Mrombo, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, aliyekutwa ameauwa huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na maeneo mbalimbali ya mwili wake, kisha mwili wake ukifichwa chini ya uvungu wa kitanda kwenye nyumba ya jirani yao.
Taarifa hii imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo, na kwamba awali mtoto huyo alikuwa ametumwa dukani toka asubuhi, lakini hakurejea na ilipofika mchana wazazi wake walianza kumtafuta maeneo mbalimbali baada ya kuingiwa na wasiwasi.
SACP Masejo amesema hadi sasa wanawashikilia watu watatu akiwepo Jaina Mchomvu Mama mwenye nyumba, ambaye amekamatwa na askari Polisi huko Mabogini Moshi, Mkoani Kilimanjaro alikokimbilia kujificha baada ya tukio hili kubaainika, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
No comments