AJIRA KWA WATOTO MASOKONI BADO NI KIZUNGUMKUTI

Mtoto Nia mwenye umri wa miaka 9 (sio jina halisi) akiwa amebeba mzigo wa mnunuzi katika Soko la Samunge Jijini Arusha. 
Mtoto Kudra (siyo jina lake halisi) mwenye mzigo begani katika Soko la Kilombero Jijini Arusha akiwa katika harakati zake za kutafuta riziki yake ya kila siku kupitia kubeba mizigo ya wanunuzi. 

Na. Vero Ignatus, Arusha. 

Utelelezaji wa Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004,ambayo  inasemani kuwa ni kosa kuajiri watoto kinyume na sheria na adhabu hutolewa chini ya kifungu cha 102 (2) ambacho kinampa Hakimu wa Wilaya na Mkazi kutoa adhabu sawa na faini isiyozidi shilingi milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa wakati mmoja kwa jinsi mahakama itakavyoona kulingana na mazingira ya kesi yenyewe. 

Hata hivyo Sheria  ya mtoto katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na sheria ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi zote zinakataza mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 kuajiriwa kufanya kazi ngumu katika maeneo ya migodi, viwanda, au mabaharia katika meli na kazi nyingine yeyote inayotambulika kama  hatarishi. 

Wazazi na walezi wanatakiwa kuzingatia wajibu wa kuwapa watoto wao malezi bora yatakayowawezesha kuwa watu wema katika jamii, kuwa wenye maono na mtazamo chanya kwa kesho waitakayo, ikianzia mtoto anapokuwa  tumboni mwa mama mpaka kufikia

No comments