ARUSHA YAWEKA REKODI YA KUWA NA PARADE REFU ZAIDI DUNIANI LENYE KUHUSISHA MAGARI YA LAND ROVER.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Leo Jumamosi Oktoba 12, 2024 ametangaza kuwa Mkoa huo wa Kaskazini mwa Tanzania umefanikiwa kuvunja rekodi ya Ujerumani iliyowekwa mwaka 2018, kwa Taifa hilo kufanikiwa kuwa na Tamasha lililokutanisha magari chapa ya Land Rover ya kuwa na magari 632.
Tamasha la Land Rover Festival 2024 lililoanza mapema leo Oktoba 12 na kutarajiwa kufikia tamati Oktoba 14, 2024 limefanikiwa kushirikisha magari chapa ya Land Rover takribani 1034, na kuweka rekodi ya kuwa na Parade ndefu zaidi duniani yenye zaidi ya Kilomita 14 ikianzia safari yake Eneo la King'ori na kutamatikia kwenye viwanja vya Magereza Kisongo Jijini Arusha.
Land Rover Festival 2024 inafanyika kwa mara ya kwanza Mkoani Arusha ikiwa na lengo la kuutangaza utalii wa Mkoa wa Arusha pamoja na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha kwa kuwa na matukio mbalimbali yatakayokusanya idadi kubwa ya watu na hivyo kuchangia kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja na la Mkoa kwa Ujumla.
No comments