Hatuwezi kubadilisha historia yetu' kuhusu biashara ya utumwa - Waziri Mkuu wa Uingereza
'Hatuwezi kubadilisha historia yetu' kuhusu biashara ya utumwa - Waziri Mkuu wa Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer ameiambia BBC "hatuwezi kubadilisha historia yetu", alipoulizwa kuhusu kulipa fidia nchi zilizoathiriwa na biashara ya utumwa.
Maoni yake yamekuja baada ya vyanzo vya kidiplomasia kuiambia BBC kwamba wakuu wa serikali za Jumuiya ya Madola wanataka kuanza "mazungumzo" kuhusu suala ambalo linaweza kuifanya Uingereza kulipa mabilioni ya pauni kwa jukumu lake la kihistoria katika biashara hiyo.
Sir Keir, ambaye kwa sasa yuko Samoa kwa mkutano wa nchi za Jumuiya ya Madola, alisema biashara hiyo ni "ya kuchukiza" na kwamba ni muhimu "kuzungumza juu ya historia yetu".
Sir Keir alisema lengo linapaswa kuwa "changamoto za leo" ikiwa ni pamoja na ustahimilivu katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kukuza biashara kati ya mataifa ya Jumuiya ya Madola.
Aliongeza kuwa ana mpango wa kusaidia nchi wanachama kufanya kazi na taasisi za fedha za kimataifa "kutoa pesa ambazo zinaweza kuwasaidia" kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Chanzo - BBC
No comments