Ukosefu wa usalama watatiza shughuli za masomo kaskazini mwa Kenya



Kwa sehemu kubwa ya muhula huu, wanafunzi wa shule ya upili ya Wajir hawajapata mafunzo kutokana na uhaba wa walimu

Wasiwasisi kuhusu ukosefu wa usalama kaskazini mwa Kenya unatishia kuvuruga shughuli za masomo. 

Walimu wengi wameomba kuhamishwa kutoka eneo hilo kufuatia visa vya kuuawa kwa walimu watatu mwezi Februari na washambuliaji wanaoshukiwa kuwa Alshabaab.

Walimu wanaotoroka wanadai wenzao waliuawa kwa misingi ya kidini. Lakini shida hii imechacha kwa miaka mitatu sasa.

Katika shule ya upili ya Wajir, wanafunzi wa kidato cha tatu wanafanya mtihani, lakini kwa sehemu kubwa ya muhula huu hakuna mafunzo yaliotolewa.
Shule hii ina upungufu wa walimu kumi na sita. Wanane walitoroka hivi maajuzi baada ya walimu watatu kuuawa katika shule moja inayopakana na Somalia.

Wanafunzi wamelazimika kujifunza wenyewe, jambo ambalo linamtia wasiwasi Mohammed Shukri, anayejiandaa kufanya mtihani wake wa kufuzu kujiunga na chuo kikuu mwishoni mwa mwaka.

'Tuna wasiwasi wa matokeo baada ya mtihani. Na unajua kwamba mwisho wa mwaka tutakuwa tunafanya mtihani sawa na wanafunzi wengine kote nchini, ambao wana walimu wa kuwafunza shuleni hivi sasa' amesema Mohammed Shukri.
Je imejitayarisha vipi kukabiliana na ukosefu wa usalama wakati wa Uchaguzi?
Shule nyingi huku zinatatizika kujaza pengo. 

Walimu waliopo wamelazimika kufundisha madarasa zaidi , huku shule nyingine zikiwaajiri walimu kwa mikataba ya muda mfupi.
Hata hivyo bado wameshindwa kuimudu hali na masomo yameathirika sana.

Walimu walianza kulikimbia eneo hili mwaka 2015, kufuatia mauaji ya zaidi ya wanafunzi 140 katika chuo kikuu cha Garissa, tukio lililowafanya walimu na wafanyakazi wengine wa umma wasio waisilamu kuhisi wako hatarini.

Mohammed Shukri - mmoja wa wanafunzi wa shule ya upili ya Wajir wanaokabiliwa na uhaba wa walimu kutokana na ukosefu wa usalama
Wachache wameanza kurejea , lakini mauaji ya walimu hivi punde katika shule moja mpakani yamezua tena wasiwasi katika eneo hili la kaskazini mwa Kenya.

Katika chumba cha kujifunza Kompyuta, kuna kompyuta 35, lakini wanafunzi hawajapata hata funzo moja la somo hili kwa takriban miaka mitatau sasa.

Mara ya mwisho kuwepo mwalimu wa somo la kompyuta hapa ilikuwa ni mwaka 2015, na tangu aondoke, hakujakuwa na mwalimu mwingine kujaza pengo hilo.
Shule ya upili ya wasichana ya Wajir
Shule ya upili ya wasichana ya Wajir iliwapoteza walimu 7 waliokuwa miongoni mwa waliokimbia.

Eneo hili ni miongoni mwa yale yanayojitahidi kuwapa watoto wa kike elimu. Sasa Mwalimu Mkuu Amaro Sylvano ana wasiwasi kuwa baadhi ya wazazi wanashinikiza kuwaozesha wasichana wao badala ya kuwarudisha shuleni

Anasema, 'Katika sehemu hii ya nchi tuna tatizo la ndoa za mapema. Kwa hiyo iwapo mzazi anaona hakuna mwalimu shuleni, kit anachofikiria ni kumuozesha bini yake.

Ni changamoto kubwa, kwa hakika baadhi yetu walimu hususan walimu wakuu tuna wasiwasi iwapo wanafunzi weut wote watarudi shuleni muhula ujao wakati mambo yatakaporudi kuwa sawa'.
Image captionWakazi wa Wajir wanasema kila Mkenya ana haki ya kuishi katika eneo hilo lakini tishio la Al Shabab linatishia kuvuruga utangamano na amani ya eneo hili
Tangu mwezi Februari Tume ya Kitaifa ya Walimu imeidhinisha zaidi ya maombi hamsini ya kuhamishwa walimu kutoka eneo hili. Jambo lililoibua pingamizi miongoni mwa wakaazi na baadhi ya viongozi wa hapa.

Lakini tume imekataa kusitisha uhamisho huo na mwenyekiti Nancy Macharia aliutetea uamuzi wake mbele ya kamati ya bunge akieleza kwamba tumechukua hatua hii sio tu Wajir ila kwa maeneo mengine ambapo walimu wanakabiliwana uhasama. Na hali itakaporudi kuwa sawa basi tutapata walimu wa kufunza.

Ameeleza kwamba kama muajiri hawawezi kuwa wanataka walimu wafanya kazi au wawajibike kila mara na wakati walimu hao wakiwa na shida basi wawapuuze. .

Wakazi wa Wajir wanasema kila Mkenya ana haki ya kuishi katika eneo hilo pasi kujali dini au kabila.

Lakini tishio la mashambulizi kutoka kwa Al Shabab linatishia kuvuruga utangamano na amani ya eneo hili

No comments