RAIS MAGUFULI:YEYOTE ATAKAYEUVUNJA MUUNGANO WETU HATUTAMFUMBIA MACHO.
Na Vero Ignatus ,Dodoma.
"Miaka 54 ya muungano wetu ni mfano wa kuigwa tuulinde,tuutunze,tuudumishe kwa manufaa ya Taifa letu"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ameipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji sambamba na kumpandisha cheo mkurugenzi Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo.
Rais wa Jamhuri Dkt. John Pombe Magufuli ametoa maamuzi hayo katika sherehe za Muungano zilizofanyika Katika uwanja wa Jamhuru Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania bara na Zanzibar pamoja na wageni mbalimbali.
Rais Katika kipindi cha miaka 54 ua Muungano Tanzania imepata mafanikio makubwaikiwemo kumeongeza maeneo ya ushirikiano hapo awali yalikuwa 11 hivi sasa yap0 22 hivyo mtu yeyote ataye jaribu kuuchezea muungano atashughulikiwa vikali hata kama atakuwa nje ya nchi ama ndani
Muungano umeifanya Tanzania kuwa na nguvu ya kuaminika Kimataifa ,kusuluhisha migogoro mbalimbali duniani hivyo hatutamfumbia mamccho mtu yeyote atakayetaka kuuvunja Muungano wetu.Alisema Magufuli.
"Miaka 54 ya muungano wetu ni mfano wa kuigwa tuulinde,tuutunze,tuudumishe kwa manufaa ya Taifa letu"
“Muungano wetu ni mfano wa kuigwa duniani, kwasababu ni muungano wa kihistoria ambao ndio muungano ambao ni mfano katika mataifa mengine, lakini kuna watu ambao hata kama mkifanya vitu vizuri wenywe kazi yao ni kubeza tu, sasa nasema kwa yeyote atayejaribu kuuchezea muungano huu atachuliwa hatua kali haijarishi yuko ndani ya nchi ama nje ya nchi,”amesema Rais Dkt.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kwenda kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshma katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika jukwa kuu kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Wananchi, Magereza na Polisi vikipita kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Kikosi cha Makomando wa (JWTZ) kikipita na kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Mmoja wa Makomando wa JWTZ akitoa Heshma kwa kupiga Saluti wakati akipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mmoja wa Makomando wa JWTZ akiwasili ndani ya uwanja wa jamhuri kwa kutumia kamba katika maadhimisho hayo ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mmoja wa Makomando wa JWTZ akionesha umahiri wake wa kuvuta gari kwa kutumia meno katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa Pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, wakati kikundi cha Halaiki kilipokuwa kikipita mbele kutoa heshma katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Askari wa Jeshi la Magereza wakionesha umahiri wa kupambana na vikwazo mbalimbali katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Spika wa Bunge Job Ndugai wakati kikundi cha vijana wa Halaiki walipokuwa wakipita mbele kutoa heshma.

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.












No comments