CHANJO YA KUJIKINGA NA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WATOTO WA KIKE(9-14) KUTOLEWA ARUSHA. APRIL 25

 Mganga mkuu wa mkoawa ArushaTimothy Wonanji akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi April 25 mwaka huu.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus blog.
Daktari Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI  Boniface Mguhuni akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na chanjo hiyo.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto mkoani Arusha akiwa anatoa elimu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusiana na chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi katika ukumbi wa Golden rose.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Dkt.Salum Msheshe kutoka ofisi ya mganga mkuu Arusha akizungunza katika semina kwa wanahabari kuhusu uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog.


Na.Vero Ignatus Arusha.


Jumla ya  Watoto wa kike 21198 wenye umri wa miaka 9-14  Mkoani Arusha wanatazamiwa kupata chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa kizazi  ambayo husababishwa na maambukizi virusi vya Papilloma.

Mganga Mkuu mkoani Arusha Timothy Wonanji ametolea ufafanuzi wa chanjo hiyo na kusema kuwa ni salama, imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mamlaka ya Chakula naDawa  Tanzania (TFDA) 


" Mwaka 2018 chanjo itatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa miaka 14 na ili kupata kinga kamili walengwa watahitaji kupatiwa dozi mbili.
Dozi ya pili itatolewa miezi 6 baada ya kupata dozi ya kwanza".alisema Timoth.

Amesema Nchini Tanzania saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza  ,ikifuatia ile ya matiti zote kwa pamoja  husababisha vifo kwa asilimia 50 vya kinamama,inaweza kusambaa na kushambulia kibofu cha mkojo,uke na sehemu za chini ya utumbo mkubwa na baadaye figo, ini na sehemu nyingine.

Kwa upande wake Daktari Mwandamizi kutoka TAMISEMI  Boniface Mguhuni ameainisha visababishi vya saratani ya mlango wa kizazi kuwa ni pamoja na kujaamiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,kuwa na ndoa za mitala,kuzaa watoto wengi pamoja na uvutaji wa sigara.


Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto mkoani Arusha Belinda Mumbuli amesema mwaka 2017 wanawake 6079 walipimwa Saratani ya mlango wa kizazi mkoani Arusha ,kati ya hao 138 walionekana na dalili za awali ,45 walipewa rufaa kwaajili ya uchunguzi zaidi

Amesema dalili za saratani  ya mlango wa kizazi kutokwa na damu bila mpangilio,maumivu ya mgongo,miguu na kiuno kuchoka kupungua uzito,kupungukiwa hamu ya kula,kutokwa uchafu kwenye uke wa majimaji uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu na kubimba miguu.


 Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea.

Dkt.Salum Msheshe kutoka ofisi ya mganga mkuu Arusha amewataka wazazi na jamii kuacha kudanganyana na kuzusha mambo ambayo yatakwamisha juhudi za kutolewa chanjo hiyo badala yake wawapeleke watoto wao wakapatiwe chanjo

Pamoja na hayo ,Wizara ya Afya mkoani hapa wamevitaka vyombo vya habari kubaini uzushi ama uvumi kuhusu chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya katika mamlaka husika na kutoa mrejesho kwenye jamii baada ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu


























No comments