WAZIRI KOMBO AWAHAMASISHA VIJANA WA TANZANIA KUCHOCHEA MABADILIKO YA MIFUMO YA CHAKULA DUNIANI
WAZIRI KOMBO AWAHAMASISHA VIJANA WA TANZANIA KUCHOCHEA MABADILIKO YA MIFUMO YA CHAKULA DUNIANI
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud
Thabit Kombo (Mb.), amekutana na vijana viongozi kutoka Tanzania
wanaoshiriki katika mageuzi ya mifumo ya chakula kupitia mradi wa Global
Alliance for Improved Nutrition (GAIN) chini ya kampeni ya Vijana4Food.
Mazungumzo
hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Mfumo wa Chakula wa
Umoja wa Mataifa (UNFSS+4) uliofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 27
hadi 29 Julai 2025 jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Kupitia
mkutano huo, Waziri Kombo amewapongeza vijana hao kwa kuwa sehemu ya
mabadiliko makubwa katika sekta ya chakula, akiwataka kutumia fursa hiyo
kuleta mawazo bunifu na kuongoza kwa vitendo mageuzi ya mifumo ya
chakula yenye lishe bora, salama na endelevu nchini Tanzania.“Nyinyi ni sauti muhimu ya vijana wa Tanzania kwenye majukwaa haya ya kimataifa. Mtumieni nafasi hii kwa manufaa ya Taifa na kuchangia maendeleo ya mifumo endelevu ya chakula,” amesema Mhe. Kombo.
Mradi wa GAIN unalenga kuwawezesha vijana kushiriki kwa dhati katika sera, mikakati na utekelezaji wa mabadiliko ya mifumo ya chakula kwa mustakabali bora wa kizazi cha sasa na kijacho.

No comments