ZALISHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI WAHIMIZWA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025
Baadhi ya wawakilishi wa serikali waliohudhuria mkutano huo.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg.Kailima Ramadhani
akitoa mada wakati wa ufunguzim wa mkutanio wa Tume na Wazalishaji
Maudhui Mtandaoni kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha
siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 03 , 2025.
Picha ya pamoja ya washirikiNa Waandishi wetu, Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa
Jacobs Mwambegele, amewahimiza wazalishaji wa maudhui mtandaoni kutumia
majukwaa yao ya kidijitali kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi
kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza
leo tarehe 03 Agosti, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni,
Mhe. Mwambegele amewapongeza wazalishaji hao kwa ushirikiano walioutoa
kwa Tume katika hatua mbalimbali za maandalizi ya uchaguzi.
Mhe.
Mwambegele amewasihi wazalishaji hao wa maudhui kuendelea kuwa daraja
muhimu kati ya Tume na wananchi kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati.
“Tuna
imani kuwa tutazidi kushirikiana nanyi kwa karibu zaidi, na mtatumia
nafasi zenu kuwapatia wananchi taarifa sahihi kuhusu maendeleo ya
maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 na kuwahamasisha kushiriki
kikamilifu kwa kupiga kura,” amesema Mhe. Mwambegele.
Amebainisha
kuwa Tume inatambua mchango wa wazalishaji wa maudhui mtandaoni katika
njia mbili kuu. Kwanza, kama daraja la mawasiliano kati ya Tume na
wadau, na pili, kama wadau wa moja kwa moja wa mchakato wa uchaguzi.
“Tume
inathamini kazi yenu ya kuandaa, kuchapisha na kusambaza taarifa
kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali kama mitandao ya kijamii,
blogu, tovuti na majukwaa ya video kama YouTube,” ameongeza.
Akizungumzia
nafasi ya vijana katika uchaguzi, Mhe. Mwambegele amesisitiza umuhimu
wa mawasiliano ya kidijitali kwa kundi hilo, akiwahimiza wazalishaji hao
wa maudhui kutumia ubunifu wao kwa kutumia michoro, video na ujumbe
wenye mvuto ili kuwafikia wapiga kura kwa njia rahisi na ya kuvutia.
Amesema
lengo kuu la mkutano huo ni kujadili hatua zilizofikiwa katika
maandalizi ya uchaguzi, kubadilishana mawazo, na kusikiliza changamoto
zinazowakabili wazalishaji wa maudhui mtandaoni ili kutafuta suluhisho
kwa wakati.
“Mkutano
huu si wa upande mmoja; ni jukwaa la mawasiliano ya pande mbili ambalo
linawapa fursa ya kueleza changamoto zenu na kusaidia kuboresha
utekelezaji wa shughuli za uchaguzi,” ameeleza Mhe. Mwambegele.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani, amehimiza
waandaaji wa maudhui mtandaoni kutumia majukwaa yao kutoa habari sahihi,
na zilizothibitishwa na kufanyiwa utafiti.
Ameongeza kuwa majukwaa hayo ya kidijitali yanasaidia kurahisisha upokeaji wa taarifa za Tume na kuwafikia wananchi kwa haraka.
Aidha,
Bw. Kailima amewahimiza wazalishaji wa mtandaoni kutoa taarifa za mara
kwa mara kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, ikiwa ni pamoja na
kuitumia kauli mbiu ya uchaguzi “Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga
Kura” ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba,
2025.
Mkutano
kati ya Tume na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni ni mfululizo wa
mikutano ya Tume na wadau wa uchaguzi ambayo ilianza tarehe 27 Julai,
2025. Mikutano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 04 Agosti, 2025 kwa
wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kupatiwa mafunzo.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani
Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutanio wa Tume na
Wazalishaji Maudhui Mtandaoni kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao
hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 03 ,
2025.
No comments