JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MAMA ANAYE TUHUMIWA MUUA MTOTO WAKE KIKATILI, WATU WENGINE
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MAMA ANAYE TUHUMIWA MUUA MTOTO WAKE KIKATILI, WATU WENGINE WAJERUHIWA
Dar es Salaam
— Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Zuhura
Juma maarufu kama Matengo kwa tuhuma za kumuua kwa ukatili mtoto wake wa
miezi saba, Shufaa Abdallah, na kujeruhi watu wengine wawili.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Polisi, tukio hilo la kusikitisha lilitokea mnamo
Juni 30, 2025, saa sita mchana katika maeneo ya Nyumbanyeupe,
Majimatitu, Wilaya ya Temeke. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alitumia kitu
chenye ncha kali kutekeleza unyama huo.
Watu
wengine wawili walioumia katika tukio hilo wametambulika kwa majina ya
Agnes Mathias na Suleiman Abdallah, ambao kwa sasa wanaendelea kupatiwa
matibabu.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema kuwa uchunguzi wa awali
unaendelea kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kisayansi ili
kubaini chanzo cha tukio hilo. Mara uchunguzi utakapokamilika, hatua
nyingine za kisheria zitafuata.
Tukio
hili limezua masikitiko na taharuki kwa wakazi wa eneo hilo, huku jamii
ikihimizwa kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa zozote
zitakazosaidia kukamilisha uchunguzi.

No comments