
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Julai 10, 2025
amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO
anayeshugulikia masuala ya Utamaduni, Bw. Ernesto Ottone, pembezoni mwa
Mkutano wa 47 wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea mjini Paris,
Ufaransa.

Kupitia
kikao hicho, viongozi hao wameazimia kukuza ushirikiano kati ya UNESCO
na Tanzania katika uhifadhi wa Maeneo ya Urithi wa Dunia yaliyopo nchini
Tanzania.

Kadhalika,
Mkurugenzi huyo ameahidi kuimarisha ushirikiano katika uendelezaji wa
shughuli za kiutamaduni nchini Tanzania na kukuza uhifadhi wa vivutio
vyake vya kipekee.

Kikao
hicho kimehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Ali
J. Mwadini, pamoja na wataalam wengine kutoka Tanzania.
No comments