RPC ARUSHA ANUSURIKA KIFO


Kamanda wa Jeshi la Polisi Arusha Charles Mkumbo amepata ajali katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya gari alilokuwa akilitumia kupasuka tairi ya nyuma na kupoteza uelekeo na kupinduka.

Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa tukio nakusema gari hilo ilikuwa na watu watatu ikiwemo Msaidizi wake pamoja na Dereva na amesema hali zao zinaendelea vizuri.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema ajali hiyo ilitokea kati ya eneo la Mdori na Minjingu wilayani Babati  jana  Februari 26  saa nane mchana.

Amesema Kamanda Mkumbo ambaye alikuwa anatoka mkoani Singida kurejea Arusha, ameumia kidole cha mkono wa kushoto na michubuko iliyotokana na kukatwa na vioo.

Amesema gari lilipata ajali baada ya kupasuka tairi la nyuma upande wa kushoto.

Ilembo amesema Mkumbo baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, aliingizwa chumba cha upasuaji moja kwa moja.

Pia, katika ajali hiyo dereva wa kamanda Mkumbo, Staff Sajent Silvanus aliumia maeneo ya paja.

Mganga mfawidhi wa Mkoa Arusha, Dk Omar Chande amesema  majeruhi wote wanapatiwa matibabu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa pia wamefika  hospitali ya mkoa kumjulia hali Mkumbo na majeruhi wengine


No comments