Mtoto wa miaka 8 afariki kwa kuzama baharini Bweleo
Mtoto wa miaka 8 aliyejulikana kwa jina la Hassan Msadiki Maneno amefariki dunia baada ya kuzama katika pwani ya Bweleo huko Wilaya ya Magharibi Unguja.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa Polisi mkoa wa mjini magharib Unguja Hassan Nassir amesema jana Februari 25, majira ya saa 4:45 asubuhi mtoto Hassan Msadiki alifariki baada ya kuzama wakati akiogelea katika fukwe za bahari ya Bweleo.
Kamanda Nassir amesema mwili wa marehemu huyo ulifikishwa hospitalini kwa uchunguzi wa madaktari ambao ulibainika kunywa maji mengi hali iliyopelekea kifo chake.
Aidha amesema baada ya uchunguzi walikabidhiwa ndugu zake kwaajili ya mazishi ambayo yalifanyika huko Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja
No comments