Home
/
Unlabelled
/
Kampuni ya Utalii ya Mwiba yatoa sh 541 milioni kuchangia miradi ya maendeleo Meatu.
Kampuni ya Utalii ya Mwiba yatoa sh 541 milioni kuchangia miradi ya maendeleo Meatu.
Arusha.
ampuni ya Utalii ya Mwiba Holdings ltd, imetoa kiasi cha sh 541 milioni katika kuchangia miradi ya maendeleo ambayo inateketezwa na Jumuiya ya Wanyamapori ya Makao na halmashauri ya Meatu mkoa wa Simiyu.Kampuni hii, imewekeza shughuli za utalii na uhifadhi katika hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya makao ambayo inapakana na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.Meneja wa miradi wa taasisi ys Friedkin conservation Fund(FCF) ambayo inasimamia miradi ya kampuni ya Mwiba, Nana Grosse-Woodley akizungumza na mwananchi, alisema fedha hizo zimetolewa katika miradi mwaka 2017 pekee.Alisema miongoni mwa miradi ambayo kampuni hiyo, imechangia mifuko 3000 ya saruji yenye thamani ya sh 48 milioni kwa ajili ya ujenzi wa miradi jamii,imetoa kiasi cha sh 32.5 milioni kuchangia miradi ya elimu."katika kipindi cha mwaka mmoja,tumetoa kwa vijiji 9 mgao jumla ya sh 89.2 milioni,tumetoa fedha za pango la ranchi kwa kijiji cha makao sh 80 milioni lakini pia tumetoa kwa halmashauri kodi pango sh 40 milioni"alisemaAlisema kupitia shughuli za utalii, katika wilaya hiyo, wametoa kiasi cha sh 28.8 milioni kwa kijiji cha Iramba ndogo,kiasi cha sh 28.8 pia kwa kijiji cha Mbushi ambapo pia kiasi kama hicho, kimetolewa kwa kijiji cha Makao.
"kwa ujumla tumetoa kias chah 541,043,519 mwaka jana pekee kama michango ya maendeleo kodi na makato mbali mbali kutokana na shughuli za utalii na uhifadhi"alisemamwenyekiti wa kijiji cha makao,Anthony Philipo alisema tangu kampuni ya Mwiba ainze kuwekeza katika kijiji chao kuna manufaa makubwa ambayo wanapata.
"wamekuwa wakichangia miradi ya maendeleo, pia wanatoka mgao wa shilingi 3milioni kwa vijiji vilivyopo ndani ya WMA kwa mwaka lakini pia kijiji chetu karibuni, tulipata mgao wa sh 10 milioni"alisema
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema uwepo wa wawekezaji katika sekta ya utalii katika mkoa wake, imekuwa ni faraja kwani licha ya kutoa fedha kwa vijiji pia halmashauri husika zimekuwa zikinufaika sambamba na serikali kuu kupitia kodi mbali mbali.
"mkoa wa Simiyu sekta ya utalii imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya wananchi na wito wa serikali ni kuhimiza maeneo yaliyohifadhiwa yaendele kutunzwa na pia kuacha kufanya uvamizi ukiwepo wa mifugo kutoka nje ya mkoa"alisema.
No comments