WATU WAWILI WAFARIKI KWA AJALI PWANI

Watu wawili ambao ni wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wamefariki dunia, huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya gari dogo aina ya Toyota Prado walilokuwa wakisafiria kutoka Mlandizi kwenda Kwala kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, amesema ajali hiyo ilitokea saa saba na nusu mchana katika eneo la Kwala na ilihusisha gari aina ya Toyota Prado mali ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, lililokuwa limebeba wataalamu waliokuwa wakifanya utafiti wa udongo katika eneo hilo.

Kamanda Morcase amesema hadi anatoa taarifa hii kwa umma majina ya waliofariki dunia pamoja na majeruhi wa ajali hiyo yalikuwa bado hayajafahamika. Ameongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.

No comments