Baraza la Usalama: Sheria za msituni zinachukua nafasi ya utawala wa sheria aonya mkuu wa UN
Baraza la Usalama: Sheria za msituni zinachukua nafasi ya utawala wa sheria aonya mkuu wa UN

- Utawala wa sheria wa kimataifa unamomonyoka
- Sheria za msituni zinachukua nafasi ya utawala wa sheria
- Wachache wanapindua kanuni kwa maslahi binafsi
- Afrika yataka ushirikiano wa kimataifa unaoaminika
- Mageuzi kwenye Baraza la Usalama si hiyari ni lazima
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limefanya mjadala wa ngazi ya juu leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kuhusu utawala wa sheria wa kimataifa huku onyo kali likitolewa kwamba hali ya kimataifa ya utawala wa sheria inakumbwa na mapungufu na Katibu Mkuu António Guterres akionya kwamba “sheria za msituni zinachukua nafasi ya kanuni za dunia zilizokubaliwa”.
Mjadala huo, uliopewa kichwa cha habari “Kuthibitisha upya hali ya sheria ya kimataifa: mikakati ya kuhuisha amani, haki na ushirikiano wa kimataifa,” umekuwa tukio kuu la urais wa Somalia katika Baraza la Usaama na umeangazia njia za kurekebisha ukiukaji wa sheria unaoongezeka na unaohatarisha uthabiti wa dunia.
No comments