UUMBI WA KUBEBA WATU 5,000 KWA WAKATI MMOJA KUJEBGWA ARUSHA KWA UBIA KATI YA AICC NA PSSSF
•Mhe. Kisuo asema mradi huo utaleta tija kidiplomasia na kiutalii Mkoani Arusha_
•Wasifu ubia wa PSSSF na AICC katika ujenzi wa Ukumbi huo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo, akiahidi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa ujenzi wa Ukumbi mkubwa wa Mikutano wa Kilimanjaro, unaojengwa Mkoani Arusha kwa ubia kati ya kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF).
Kulingana na Mhe. Makalla katika mazungumzo yao leo Jumanne Januari 06, 2025 ofisini kwake Jijini Arusha, amesema Mkoa wa Arusha ni kitovu cha utalii kwa Kanda ya Kaskazini na ndio mwenyeji wa Mikutano mingi ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kujengwa kwa Ukumbi huo kutachochea na kukuza hadhi ya Mkoa katika sekta ya utalii na Mikutano na hivyo kusisimua uchumi wa wananchi wa Arusha.
"Nimeambiwa kuwa Ukumbi ule wa kisasa utakuwa na uwezo wa kubeba watu 5,000 kwa wakati mmoja, kutakuwa na kumbi zisizopungua 40 na kutakuwa na eneo la maonesho litakaloweza kuhudumia watu 10, 000. Mkandarasi kuoneshwa eneo bila shaka sasa baada ya ziara yako Mhe. Naibu Waziri ni kazi kuanza na tuahidi ushirikiano na kusimamia hilo kikamilifu." Amesema Mhe. Makalla.
Kwa upande wake Mhe. Kisuo aliyeambatana na Menejimenti ya PSSF amesema ni matumaini yake kuwa ushirikiano wa Wizara na Mkoa utafanikisha ujenzi huo, akisema kukamilika kwa mradi huo wa kimkakati kutaongeza tija kwenye sekta ya utalii, diplomasia na sekta nyingine za kiuchumi, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Fortunatus Magambo kwa ubunifu na ubia wa PSSF na AICC.
No comments