AWAMU YATATU YA NG'ARISHA JIJI ARUSHA YAZINDULIWA

Leo January 24.2026 Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maxmillian Matle Iranqhe amezindua awamu ya tatu ya kampeni ya 'NG'ARISHA JIJI' katika kata ya Daraja II kampeni ambayo inalenga kuhamasisha usafi wa Mazingira wa Maeneo yote ya Jiji.

Akihutubia Wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa Kampeni hiyo kwa kuendesha zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Kituo cha Afya Daraja II Meya Maxmillian amewaelekeza Watendaji wa kata kuwasimamia Maafisa afya kusimamia kikamilifu zoezi la Usafi wa Mazingira katika maeneo yao kila mara na isiwe tu wakati wa Jumamosi ikiwa sambamba na kuwapa elimu ya utunzaji wa Mazingira Wananchi kwa kufanyia usafi mazingira yao ya biashara na makazi kabla ya kufungua biashara na Jioni baada ya kufanya biashara

No comments