Wajasiriamali/Wafanyabiashara wadogo Wapatiwa Elimu juu ya Uwezeshaki wa Ki biashara katika eneo la Viwanda SIDO Jijini Arusha.
Meneja Mkoa TRA Arusha Bw. Deogratius Shuma leo tarehe 27 Agosti 2025 akizungumza na Wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara wadogo katika eneo la Viwanda SIDO Jijini Arusha.
Afisa Mkuu Elimu na Mawasiliano TRA Arusha Eugenia Mkumbo akizungumza na Wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara wadogo katika eneo la Viwanda SIDO Jijini Arusha leo tarehe 27 Agosti 2025
Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti Wa wafanyabiashara eneo la viwanda SIDO Aloyce Samson Kingcolla akiwa na baadhi ya washiriki katika program maalum ya mwendelezo wa Dawati la Uwezeshaji Biashara kwa Wafanyabiashara Jijini Arusha.
Washiriki katika program maalum ya mwendelezo wa Dawati la Uwezeshaji Biashara kwa Wafanyabiashara Jijini Arusha ilitozinduliwa tarehe 27/8/2025 na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Mwenda
Meneja Mkoa TRA Arusha Bw. Deogratius Shuma akimuhudumia mteja katika maeneo ya Viwandani SIDO Jijini Arusha.
Na. Vero Ignatus, ARUSHA
Meneja Mkoa TRA Arusha Bw. Deogratius Shuma tarehe 27 Agosti 2025 ameendesha program maalum ya mwendelezo wa Dawati la Uwezeshaji Biashara kwa Wafanyabiashara lililozinduliwa na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Mwenda hapo 26 Agosti 2025
Zaidi ya washiriki 200 wamehudhuria katika program hiyo ambapo inaashiria hatua muhimu katika juhudi za Serikali ya Tanzania za kukuza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara, hasa wale wa sekta isiyo rasmi, na kuhakikisha wanapata nafasi ya kuchangia uchumi wa taifa
Shuma amesema kuwa hiyo Programu imehusisha huduma ya mtu kwa mtu ambayo ameiongoza yeye, pamoja na Meneja Msaidizi Huduma ikiambatana na utoaji elimu ya kodi kwa Wafanyabiashara wa eneo la Viwanda SIDO, pamoja na Wanafunzi Wajasiriamali walioko chini ya program ya Mafunzo inayoendeshwa na SIDO
Afisa Mkuu Elimu na Mawasiliano TRA Arusha Eugenia Mkumbo amesema kuwa aliweza kuwaelimisha wafanyabiashara hao wadogo namna ya kuingia kwenye mfumo na kuangalia taarifa zao kama kuna mahali waoichelewa ama kucheleweshwa.
Bi Mkumbo akijibu swali lililoulizwa na mmoja wajasiriamali juu ya Kodi ya Taasisi/NGO alisema Mtu akiwa na Taasisi lazima awe na TIN namba yake yenyewe, vile vile inajikadiria Kodi yenyewe kwa njia ya mtandao, ambapo mkurugenzi mmojawapo atawajibika kuwasilisha kila mwezi return kwa njia ya mtandao ikiwemo taarifa ya waajiriwa au wakurugenzi, taarifa ya mwaka pamoja na hesabu za mwaka mzima.
Bi.Mkumbo alisema serikali imerahisisha namna bora ya uapatikanaji wa mashine ndipo TRA ikaja na mfumo rahisi wa utengenezaji mashine za utoaji mashine risiti zisizo na gharama kubwa ambapo zipo katika mfumo wa kidigitali unaounganishwa kwenye simu za kiganjani tofaiti na ilivyokuwa happy awali machine za EFD Ilikuwa Inauzwa ghali jambo ambalo mfanyabiashara mdogo Ilikuwa vigumu kuinunua.
Kwa upande wake. Mwenyekiti wa wafanyabiashara maeneo ya SiDO bwana Alex Samson Kingcolla ameishukuru Mamlaka ya Mapato TRA kwa kuzindua dawati hilo na kuwapatia elimu ya mlipa Kodi kwao ni fursa kubwa itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi hadi kukua na kuwa wafanyabiashara wakubwa
Aidha amesema wanepata elimu juu ya uuzaji na ununuzi wa wa magari kwamba lazima wabadilishe umiliki tofauti na awali wali kuwa wanapewa kadi huku Deni likisalia kwa mmiliki wa kwanza
No comments