WAAJIRI WAASWA KUHESHIMU SHERIA NA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI.

 Na Mwandishi Wetu,  Arusha.Septemba-15-2025

Waajiri nchini wametakiwa kuweka utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wao kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara yatakayowawezesha kuwa na uelewa wa pamoja na hivyo kuepusha migogoro sehemu za kazi.


Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Bi. Zuhura Yunus, alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE uliofanyika leo, Jumatatu, tarehe 15 Septemba 2025, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha.


Kauli ya Bi. Zuhura Yunus

Akizungumza katika semina hiyo, Bi. Yunus alisema:

“Watumish


Aidha, aliwaonya baadhi ya waajiri kuacha tabia ya kuwazuia watumishi kujiunga na vyama vya wafanyakazi, akisisitiza kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki zao za msingi. Aliongeza kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua mwajiri yeyote atakayebainika kukiuka sheria hiyo.

Salamu za TUGHE

Awali, akitoa salamu za ukaribisho, Katibu Mkuu wa TUGHE, Cde. Hery Mkunda, alisema idadi ya washiriki wa semina imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mwaka huu 2025, TUGHE inatarajia kutoa mafunzo kwa washiriki zaidi ya 800 kutoka Wizara, Idara, Taasisi, Wakala wa Serikali, Bunge, Mahakama, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Taasisi za Afya za umma na binafsi.

Mkunda alibainisha kuwa mafunzo haya, yaliyoanza rasmi mwaka 2018, yanalenga kutoa elimu ya kiutumishi kwa waajiri, watumishi na wanachama wa TUGHE, huku yakiwa na lengo la kuimarisha mahusiano mema baina ya waajiri na wafanyakazi ili kupunguza migogoro sehemu za kazi.

Viongozi Waliohudhuria



Ufunguzi wa semina hiyo ulihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo:


  • Kamishna wa Kazi, Mhe. Suzan Mkangwa
  • Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Yose Mlyambina
  • Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri, Mhe. Vallensi Wambali
  • Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Mhe. Usekelege Mpulla
  • Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Cde. Joel Kaminyoge
  • Makamu Mwenyekiti TUGHE Taifa, Dkt. Jane Madete

Kuhusu Mafunzo

Mafunzo haya yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Alhamisi, 18 Septemba 2025, ambapo washiriki wote watashiriki katika utalii wa ndani kwa kutembelea Mlima Kilimanjaro kabla ya kupatiwa vyeti vya ushiriki.






No comments