DAR-ES-SALAAM : SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeondoa sokoni tani 42 za bidhaa za chakula za watoto maarufu chama zenye ‘mido li’ ndani yake. 

Pia, limesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini uwepo wa viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo, ilipiga marufuku na kusitisha 
uzalishaji na uingizwaji wa bidhaa hizo sokoni. 

Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa TBS, Kandida Shirima alitoa ufafanuzi huo wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari uliofanyika jana kuelezea mafanikio ya TBS katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita. 

Alisema shirika lilibaini uwepo wa baadhi ya wazalishaji wanaofunga vyakula na vitu vingine kama midoli hasa kwenye bidhaa za chakula za watoto kwa lengo la kuvutia watumiaji. 

Alisema baadaye walichukua hatua ya kutoa taarifa kwa umma na kuvifikia vi wanda vinavyozalisha bidhaa hizo na kusitisha uzalishaji wake. “Tumefanya ukaguzi kupitia ofisi zetu za kanda nchi nzima na tumeziondoa kwenye soko tani 42 tumeendelea kusitisha uzalishaji na sasa hakuna anayezalisha,” alisema. 


Credit -Habarileo

No comments