TUME YA UCHAGUZI YAPONGEZWA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2025
TUME YA UCHAGUZI YAPONGEZWA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2025
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kilichokutana Mjini Unguja Zanzibar leo
Juni 9,2025.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi la Tume akizungumza mapema kabla ya ufunguzi wa
kikao hicho.
Wajumbe wa Baraza hilo wakifuatilia mada katika Mkutano huo.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz
(kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la
Tume, Ramadhani Kailima, wakati Katibu Mkuu huyo alipofika kufungua
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Tume Mjini Unguja, Zanzibar leo Juni
9,2025.Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz
(kushoto) na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Tume, Ramadhani
Kailima, pamoja na wajumbe wa baraza la Wafanyakazi la Tume wakiimba
wimbo wa wafanyakazi wakati kabla ya kuanza kikao cha Baraza la
Wafanyakazi Mjini Unguja, Zanzibar leo Juni 9,2025.

Na. Mwandishi Wetu, Zanzibar
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge
na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa
kukamilisha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na
kuendelea vyema na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Dkt. Yonazi ametoa pongezi hizo leo tarehe 09 Juni, 2025 Kisiwani Unguja, Zanzibar wakati wa kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la INEC, ambapo imewaasa viongozi wa Tume kuendelea kuwa imara na kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unakwenda vizuri.
“Kwanza niwapongeze sana kwa kukutekeleza jukumu hili kubwa ambalo mmekabidhiwa na Taifa letu na kwa namna ya pekee kabisa Mwenyekiti wa Baraza unifikishie salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele pamoja na wajumbe wa Tume kwa kazi kubwa ambayo mmeifanya katika kuhakikisha kuwa shughuli za uchaguzi nchini kwetu zinakwenda vizuri,” amesema Dkt. Yonazi.
Ameeleza kuridhishwa na jinsi Tume ilivyotekeleza kwa ufanisi zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuongeza kuwa ni matarajio ya Serikali kuwa utendaji huo mzuri wa Tume utaendelea kwa viwango vya juu kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu mbalimbali ambazo zimewekwa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu. Kailima Ramadhan amesema tayari Tume imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo kwa sasa inaendelea na uboreshaji wa awamu ya pili.
“Tume imeshakamilisha uboreshaji wa awamu ya kwanza na imeshachakata na kutoa daftari la awali na imeshakamilisha uboreshaji wa awamu ya pili mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili. Tunategemea kuanzia tarehe 28 mwezi huu (tarehe 28 Juni, 2025) tutaanza mzunguko wa tatu wa uboreshaji katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar na Magereza Tanzania Bara kwa wanafunzi na wafungwa waliohukumiwa kifungo chini ya miezi sita,” amesema Kailima.
Katibu huyo wa Baraza amesema mzunguko huo wa tatu utahusisha vituo 140 vya kuandikisha wapiga kura ambapo 130 vipo kwenye magereza Tanzania Bara na vituo 10 vipo kwenye vyuo vya mafunzo Tanzania Zanzibar. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku saba hadi tarehe 04 Julai, 2025.
Ameongeza kuwa Tume imekamilisha maandalizi ya nyaraka mbalimbli kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni pamoja na Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 na maelekezo mbalimbali kwa ajili ya watendaji wa uchaguzi na wadau wa uchaguzi kupata miongozo kwa ajili ya utekelezaji wa uchaguzi.
Alimkumbusha mgeni rasmi kuwa tayari Tume imekamilisha zoezi la ugawaji wa majimbo na kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutakuwa na jumla ya majimbo 272 yatakayofanya uchaguzi wa wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kata 3960 kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara.





No comments