Tanzania Kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani Kitaifa Mjini DodomaHabari

Tanzania Kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani Kitaifa Mjini Dodoma

Na. Vero Ignatus, Arusha 

Tanzania kuungana na nchi nyingine duniani Kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani ambapo Kitaifa itafanyika Mjini Dodoma makao makuu ya nchi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arusha Katibu tawala wa wilaya ya Arusha Jacob Julius Rombo,Mara baadaa ya usafi wa mazingira jijini hapa 31mei 2025 amesema Maadhimisho hayo yana umuhimu mkubwa kwani yanatoa fursa ya kutafakari hali ya mazingira huku ukizingatia  kuhamasisha jamii kuchukua hatua madhubuti katika kuyalinda na kuyatunza. 

Rombo amesema Maadhimisho hayo hujumuisha shughuli mbalimbali za upandaji miti, usafishaji wa maeneo mbalimbali, na mijadala ya kitaalamu kuhusu mikakati ya kukabiliana na changamoto za mazingira, umuhimu wa katika maendeleo ya nchi, ukizingatia changamoto za mazingira kama vile ukataji miti, uharibifu wa vyanzo vya maji, na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoikabili sehemu mbalimbali za Tanzania.

"Siku ya Leo tarehe 31/5/2025 Jiji la Arusha katika kuelekea katika siku hii Sisi tumefanya usafi katika maeneo ya soko kuu, stend kuu ya mabasi Lego kiliwa ni kuhamasisha u muhimu wa siku hii, Sisi tutayo sheria ndogo inayohusu mazingira ukikutwa na uchafu katika eneo ambalo unafanyia kazi zako ofisi yako utatozwa faini shilingi 50,000,hivyo kila mmoja wetu atilie suala ya kuweka mazingira safi maanani na iwe ndiyo tabia siyo hadi ulazimishwe"alisema

Akizungumza kwa niaba ya Meya wa Jiji la. Arusha Diwali wa kata ya Ngarenaro Doita  Isaya Harry wananchi amewataka  kuakikisha maeneo yako ya biashara yanakuwa  safi na yenye kuvutia kwa ni hakuna mtu yeyote wakuja kukufanyia usafi kwenye eneo la mtu mwingine ni aibu

Doita amesema suala la usafi ni jambo la msingi Sana hivyo mwananchi yeyote katika Jiji la Arusha na Viunga vyake anatakiwa akae sehemu safi na yenye he was safi 

"Kata zote 25 mitaa 154 mabalozi wote na wajumbe wao, madiwani watendaji wetu wote na Jamii kwa ujumla  viongozi wa vyama. Vya siass hakikisheni MBA kuwa katika mazingira safi. Bila kusimamiwa mjisimamia wenyewe"

Kwaupande wake mwananchi aliyeshiriki katika zoezi la usafi wa mazingira bi Grace pallangyo amesema Kwa uwepo wa Mheshimiwa Rais,kitaifa Dodoma inatarajiwa kuwa ujumbe mzito utatolewa kuhamasisha wananchi, taasisi za serikali, sekta binafsi, na mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana katika juhudi za uhifadhi wa mazingira. 

Vilevile Kupitia maadhimisho haya Dodoma, Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kutoa wito wa pamoja wa kuchukua hatua za haraka na madhubuti ili kulinda sayari yetu.Kila mmoja wetu ana jukumu l kutunza mazingira yetu, na Siku ya Mazingira Duniani inatukumbusha wajibu huo.

Maadhimisho haha yamebeba kaulimbiu isemayo Kampeni Dhidi ya Uchafuzi wa Plastiki - Tushirikiane Pamoja Kuahidi Kuokoa Sayari ya Bluu kwa Wakati Ujao Mzuri ."

Ikumbukwe kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikionyesha dhamira thabiti katika kulinda mazingira kupitia sera, sheria, na mipango mbalimbali. Siku ya Mazingira Duniani inatoa jukwaa la kuongeza kasi ya utekelezaji wa mipango hii na kuhamasisha ushiriki mpana wa wananchi katika kutimiza azma ya kuwa na nchi yenye mazingira safi, salama na endelevu kwa vizazi 









No comments