
Katikati ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa PPRA Denis Simba wakiteta jambo wakati akiwasili katika Kituo cha kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha Kwaajili ya Kongamano LA 9 la ununuzi wa Umma 2025.
Mkurugenzi mkuu wa PPRA PPRA Denis Simba wakiteta jambo wakati akizungumza na washiriki wa Kongamano LA 9 la ununuzi wa Umma 2025. katika ukumbi wa Simba katika Kituo cha kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha
Washiriki zaidi ya 1500 wa Kongamano 9 la ununuzi wa UMMA lililofanyika Jijini Arusha katika Kituo cha kimataifa cha AICC June 13,2025
Na Vero Ignatus, Arusha
TAASISI ZA UNUNUZI WA UMMA ZAASWA KUTEKELEZA TAKWA LA KUTENGA ASILIMIA 30% KWAAJILI YA MAKUNDI MAALUM
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amefungua Kongamano la 9 la ununuzi kwa umma leo June 14,2025 Jijini Arusha ambapo amemuwakilisha Waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Mchemba likiwa na kauli mbiu isemayo ununuzi wa Umma Kijidigitali kwa maendeleo endelevu ukuzaji wa kampuni za wazawa na makundi maalum kwa ukuaji wa uchumi jumuishi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Dkt Gwajima alizielekeza Taasisi za ununuzi za umma nchini kutenga asilimia ya ununuzi wao wa mwaka kwa ajili ya kampuni za wazawa na makundi maalum,
Kuzingatiaji matumizi sahihi ya mifumo ya kidigitali katika Ununuzi wa umma nchini, Halmasahuri zote nchini zisaidie kuibua makundi maalum, kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi
(Wataalam wanaohusika katika shughuli za ununuzi mzingatie weledi wa taaluma
"Serikali ilifanya maamuzi kwa kupitia Sheria za Ununuzi wa Umma kuhakikisha tunakuza biashara ndogo, za kati, na za ndani kupitia mipango ya uhifadhi na upendeleo Kadhalika, Serikali pia imeweka masharti kwenye Sheria ya Ununuzi
wa Umma ya kutenga asilimia 30 ya fedha zinazotumika kwenye Ununuzi kwa makundi maalum ikiwemo vijana, wazee, wanawake na watu wenye mahitaji maalum."alisema
Vilevile alisema Tanzania imetambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika ununuzi wa umma, kwani mifumo hii kwa kiasi kikubwa inaondoa
changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele kwenye sekta hiyo jambo ambapo lilipelekea Serikali kupitia Wizara ya Fedha ikaamua kujenga Mfumo mpya
wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (National e-Procurement system of Tanzania –NeST) ambao unasimamiwa na PPRA.
"PPRA ilianzishwa kwa malengo ya kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya fedha katika ununuzi na ugavi; kuhakikisha uzingatiaji wa haki, ushindani,uwazi uendelevu, uwajibikaji, matumizi mazuri ya fedha, ufanisi na uadilifu katika ununuzi na ugavi; kuweka viwango vya mifumo ya ununuzi wa umma na ugavi katika Nchi kuhakikisha taasisi nunuzi zinatoa upendeleo kwa wazabuni wa ndani katika zabuni za bidhaa, kazi za ujenzi na
huduma; kwa kuzingatia sheria kujenga uwezo katika ununuzi na ugavi" Alisema
Denis Simba ni Mkurugenzi mkuu wa PPRA amesema mfumo wa NeST umeleta mageuzi makubwa katika kutekeleza dhima ya Serikali ya kuwa na Ununuzi endelevu hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,ambapo Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 pekee, utafiti wa awali uliofanywa na Mamlaka umebaini, mfumo huo umepunguza metariki tani 617.85 za utoaji wa kaboni angani, umetokana na kupunguza kiasi kikubwa matumizi ya karatasi, Kiasi hicho cha uokoaji ni sawa na kuondosha magari 144 yanayotumia mafuta ya diseli barabarani kila mwezi.
"Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka, 2023 imejumuisha masuala mbalimbali ambayo yana faida na manufaa makubwa kwa Taifa. Masuala hayo ni pamoja na kuhakikisha taasisi nunuzi zinatoa upendeleo kwa wazabuni wa ndani katika zabuni za bidhaa, kazi za ujenzi na huduma. Pia, kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, Taasisi nunuzi zimeruhususiwa kutoa upendeleo kwa ushirika, ubia au mikataba midogo iliyoingiwa baina ya kampuni za ndani na kampuni za kigeni. Alisema.
Simba amesema Mamlaka imeendelea kutoa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa NeST na kuwezesha kusajili kwa Makundi Maalum. Tangu kuanza kutumika kwa mfumo hadi sasa vikundi 578 vimesajiliwa na kuanza kutumia mfumo wa NeST, na kuomba zabuni zinazotolewa na taasisi za Serikali.Hadi sasa jumla ya tuzo 501 zenye thamani ya Shilingi 16.1 Bilioni zimetolewa kwa Makundi Maalum.
"Hivyo mnamo mwezi Novemba, 2024 Tanzania, kupitia mfumo wa NeST, ilipata tuzo ya miradi bunifu Afrika iliyotolewa na Umoja wa Afrika kupitia APA, nchini Uganda, tarehe 05 Juni, 2025 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, PPRA ilipatiwa tuzo ya heshima kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ya uchangiaji wa utunzaji wa mazingira kutokana na matumizi ya mfumo wa NeST. "Alisema Simba.
Kwa upande wake Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga amesema kuwa uzingatiwaji wa Sheria utaweza kupunguza kiwango cha upotevu wa mali na kuchukua hatua ambazo zimewekwa katika Sheria ili kukomesha mambo ambayo ni kinyume na matarajio ya Serikali na kuhakikisha kwamba fedha za umma zinalindwa kadiri inavyowezekana.
Dkt. Mwakibinga alisema, kongamano hilo muhimu limekutanisha, Wadau wa Ununuzi wa Umma kwa maana ya Watendaji wa Umma, Makampuni, Viongozi, Wafanyabiashara na watu mbalimbali ili kufanya majadiliano ya kujenga himaya ya Ununuzi wa Umma iliyo thabiti.
"Kama mnavyofahamu ununuzi wa umma ni moja kati ya nyenzo zinazotumika kwa manufaa mbalimbali ikiwemo kuutumia ununuzi wa umma kwa kuzinufaisha kampuni za wazawa ili ziweze kukua na kuwa na mchango katika maendeleo ya nchi, kuyajali makundi mbalimbali ya jamii ambayo yakiachwa bila kusaidiwa au kuwezeshwa yanapata ugumu katika ushindani wa soko la ununuzi wa umma.” Alisema Dkt. Mwakibinga
Vile vile ufunguzi huo ulikwenda sambamba na utoaji wa tuzo na zawadi kwa kwa ambazo zimetekeleza takwa la kutenga asilia thelathini (30%) kwa ajili ya makundi maalum. Vigezo mbalimbali viliwekwa kwa ajili ya kuwapata washindi ikiwemo kuangalia ni asilimia ngapi ya tuzo ambazo Taasisi nunuzi imeshatoa hadi kufikia mwezi Juni, 2025.
Mwisho
No comments